Nasibu Abdul Jumaa ‘Diamond Platnumz’ na Wema Isaac Sepetu katika pozi.
Yule
kigogo au taita aliyekuwa akimpa jeuri ya fedha Wema Isaac Sepetu
ajulikanaye kwa jina moja la Clement anadaiwa kutangaza vita na staa wa
Bongo Fleva, Nasibu Abdul Jumaa ‘Diamond Platnumz’.Habari ‘hoti’ zinadai kuwa Clement anataka Diamond arudishe gharama alizomgharamia Wema ndipo waendeleze mapenzi yao.Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa kigogo huo, Clement anadai kwamba gharama alizotumia kwa Wema ni kubwa mno lakini bidada hakujali chochote na kuukabidhi moyo wake kwa ‘Mtoto wa Tandale’ ambaye ndiye barafu wa moyo wake.
“CK (Clement) anaumia sana kuona kuwa ameteketeza fedha nyingi kwa Wema lakini bila hiyana, mrembo huyo akabwaga manyanga kisha akarudisha mpira kwa kipa na kuanza moja huku kaka mkubwa akiachwa kwenye mataa,” alitonya mnyetishaji huyo bila kufafanua kama Clement aliachwa mataa ya eneo gani.
Akiendelea kutiririka bila kuweka nukta au ya mkato, mtu huyo alisema kuwa kiasi ambacho kinadaiwa kuteketea kwa Wema kinakaribia Sh. milioni 279.6 ambazo gharama hizo zinahusisha vitu kadhaa alivyowekeza kwa Wema.
“Kuna gharama za utengenezaji wa Filamu ya The Super Star ambayo haijulikani kilichotokea kwani hadi leo haionekani sokoni.
“Kama hiyo haitoshi kwenye uzinduzi wa filamu hiyo akamleta staa wa filamu wa Nollywood, Nigeria, Omotola Jalade Ekeinde na sherehe mbili za uzinduzi zilifanyika katika hoteli kubwa mbili tofauti, ikasemekana milioni arobaini na nane ziliteketea.
“Kuna kodi ya pango la ofisi ya Wema ya Endless Fame iliyopo Mwananyamala Koma-koma, Dar, jamaa alilipa milioni nane na laki nne kodi ya miaka miwili ambayo kwa mwezi ni laki tatu na nusu.
“Ukiachana na gharama za nyumba na ofisi, kuna gari aina ya Audi Q7, inadaiwa kanunua Clement kwa Sh. milioni 98, Toyota Harrier Lexusya Sh. milioni 48 na Toyota Mark X iliyomtoa Sh. milioni 25.
“Usisahau hata lile Toyota Noah ‘kitimoto’ la ofisi alinunua Clement kwa Sh. milioni 10, faini aliyolipiwa
Kajala Masanja mahakamani Sh. milioni 13, gharama za kuirekebisha ngozi yake alipoenda nchini China iligharimu Sh. milioni 14, yaani jumla ni kama Sh. milioni 279 na ushee. Na hiyo ni kwa vitu vinavyojulikana ukiachia mbali shopping za Dubai,” alitiririka kikulacho huyo.
Baada ya kujazwa data, Risasi Jumamosi lilijaribu kumtafuta kigogo huyo lakini licha ya juhudi zote hizo hakuweza kupatikana ndipo alipogeukiwa Diamond:
“Sitishiki kwa lolote lile kwani huko nyuma kabla sijawa maarufu kivile enzi ya Nenda Kamwambie (wimbo) niliwahi kukaa mahabusu kwa siku kadhaa na sababu ilikuwa mapenzi kwa hiyo kwa hili siogopi kitu kwanza mimi ndiyo alinichukulia na mwana mpotevu amerudi kundini,” alisema Diamond anayekimbiza na Ngoma ya Number One