WATU
wanne wapo katika hali mbaya na wengine saba wamejeruhiwa baada ya lori
scania namba T653 BFD (scania 380) kugongana uso kwa uso na baso dogo
la abiria Toyota Hiace T613 CPG iliyokuwa inatoka mbagala kwenda
mkuranga.
Kwa
mujibu wa shuhuda ya ajali hiyo iliyotokea Mwandege, Dominic Kubhota,
ameiambia blogu hii usiku huu kwamba chanzo cha ajali hiyo ni ovateki
isiyotumia akili ya lori hilo .
Majeruhi hao
wamefikishwa katika hospitali ya Mkuranga, lakini muda mfupi baadaye
walianza kukimbizwa kuleta dare s salaam kw amatibabu zaidi.
Abiria wawili waloikuwa mbele ya daladala walikatika miguu.
Majeruhi wengine walioweza kuzungumza ni:
Mustafa mfungapoa wa mkuranga
Abdul Ally wa mwandege
Ramadhani rajab
Theofrida Mwinuka ( alikuwa mbele amevunjika miguu)
Jamal mbaraka ( aliyekwanguka ngozi ya kichwa)
Abraham Mohamed
Swalehe salum
NA LUKWANGULE