Home »
Uncategories »
YAMETIMIA:. LULU, BWANA’KE WAMWAGANA
YAMETIMIA:. LULU, BWANA’KE WAMWAGANA
Unknown
8:55 AM
Na Gladness Mallya LILE
penzi la msanii wa filamu na mtangazaji, Lulu Mathias na mchezaji mpira
wa zamani, Amani limesambaratika baada ya hivi karibuni mwanaume huyo
kuondoka na kilicho chake huku akimwacha mwanadada huyo ndani ya nyumba
peke yake.
Msanii wa filamu za Kibongo Lulu Mathias.
Chanzo chetu makini kilisema kuwa, tukio hilo lilitokea hivi karibuni
huko Majohe walipokuwa wakiishi wawili hao ambapo mwanaume huyo aliamua
kuondoka na kurudi nyumbani kwao na kumuacha Aunty Lulu ndani ya nyumba
hiyo waliyokuwa wamepanga.
Baada ya kuzipata habari hizo, paparazi wetu alimtafuta Aunty Lulu, akafunguka:
“Ukweli mimi na Amani tumeachana kwani kipigo kimenizidi kila kukicha
isitoshe ndugu zake hawanipendi, nimebaki peke yangu kwenye nyumba
tuliyokuwa tumepanga huku Majohe na yeye ameondoka na vitu vyake vyote,
amerudi kwao.”