Rais
wa Kenya,Uhuru Kenyatta akitoa hotuba yake katika Ikulu ya Nairobi
wakati wa hafla ya kuiaga timu ya Taifa ya Kenya Harambee Stars aliyoipa
ofa ya kwenda ziara ya mafunzo kwenye Kombe la Dunia nchini Brazil.
Rais Kenyatta akiongea na wachezaji wa Harambee Stars.
Rais Kenyatta akigawa tiketi kwa wachezaji huku akishuhudiwa na mkewe Margaret Kenyatta na Seneta wa Nairobi Mike Sonko (kushoto).
Rais Kenyatta, mkewe Mama Margaret Kenyatta na Seneta wa Nairobi Mike Sonko wakipozi Ikulu ya Nairobi na Harambee Stars wakati wa hafla hiyo fupi ya kukabidhi tiketi za ndege za kuendea Brazil kuona kombe la dunia.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameizawadi kwa
kuifadhili timu ya taifa ya soka Harambe Stars ziara ya kwenda Brazil
kutazama michuano ya kombe la dunia Hafla ya kuikabidhi rasmi ufadhili
huo timu hiyo, ilifanyika katika ikulu ya Rais Ijumaa ambapo wachezaji
kumi na moja wa timu hiyo walikabidhiwa tiketi za ndege kwenda Brazil.
Kitendo cha Rais bila shaka ni jambo la
kutaka kuwatia motisha wachezaji wa timu ya taifa ambao hivi karibuni
waliicharaza Djibouti mabao mawili kwa moja katika duru ya kwanza ya
michuano ya kuwania kombe la taifa bingwa Afrika baadaye mwakani.
Mmoja wa wachezaji hao alifurahi sana na
kusema kuwa hatua ya Rais Kenyatta kwao imetimiza ndoto yao. Rais
atagharamia tiketi za timu hiyo kutazama michuano, malazi na usafiri
ingawa haijulikani ni mechi zipi watakazotazama.
Hatua ya Rais Kenyatta imewashangaza watu
wengi sana nchini Kenya kwa kuwa timu ya taifa ya Kenya haikuwahi kufuzu
kushiriki michuano hiyo, sasa wengi wanahoji hatua yake itasaidia nini?
Soka ya Kenya imekuwa ikikumbwa na changamoto si haba, usimamizi duni
na wachezaji kukosa motisha ya kufanya vyema kwa ajili ya usimamizi huo
mbaya.
Kenyatta na mkewe mama wa kwanza wa taifa Margaret Kenyatta wamewafadhili vijana hao kwa kima cha dola elfu arobaini.
Akitoa ufadhili huo Kenyatta amesema lengo
lake hasa ni kuwapa matumaini na motisha ya kuweza kuinua mchezo wa soka
nchini Kenya.
Pia ni kama ishara ya kuthamini wachezaji hao ambao hivi karibuni walishinda kombe la Cecafa.
Kenyatta mwenyewe hatakwenda na kikosi hicho bali amewaasa vijana hao kuwa mabalozi wema wa Kenya nchini Brazil. Ufadhili huu unakuja miezi sita baada ya Kenyatta kukubali kumlipa mshahara wa kocha wa timu hiyo kwa miakja miotano ijayo.

Kenya haijawahi kufuzu kwa michuano ya
kombe la dunia lakini ziara hii kwa vijana wa Harambee Stars itawafungua
macho huku wakiwa na azma ya kufuzu kwa michuano ya taifa bingwa Afrika
mwaka 2015 baada ya kufuzu kwa duru ya pili na kujiandaa kuchuana na
Lesotho tarehe 18 Julai. BBC