Marehemu Mariagoreth Enock Ndangio |
Mama yetu Mpendwa, leo umetimiza mwaka mmoja (25 Novemba 2012) tangu ulipoitwa ghafla na Mwenyezi Mungu aliye juu Mbinguni na mkuu na muweza wa yote duniani na mbinguni.
Tunakukumbuka kwa mengi sana hasa malezi bora kwetu, elimu, ushauri, ucha Mungu na mengine mengi.
Kila mmoja wetu, kwa namna ya kipekee, anakumbuka upendo wako wa dhati kwetu sisi wote, wanao na wakwe zako bila ya ubaguzi wowote. Upendo wako kwetu umekuwa nuru na mfano wa kuigwa nasi na umetufanya tushikamane na kupendana sana na tunamuomba Mwenyezi Mungu ili tudumu kwenye mshikamano na upendo huo.
Unakumbukwa sana na mumeo mpendwa, Enock Mbalahami, mtoto wako – Derick, mama yako Honoratha Steven wadogo zako Bertha Ndangio, Daniel pamoja na ndugu, jamaa na marafiki.
RAHA YA MILELE UMPE EE BWANA NA MWANGA WA MILELE UMWAANGAZIE.
APUMZIKE KWA AMANI, AMINA.