Na Mwandishi wetu
Mwanamke
mmoja ameuawa kikatili kwa kukatwa katwa na mapanga sehemu mbalimbali
za Mwili wake kwa kudhaniwa kuwa anaimani za Kishirikina, Mwanamke huyo
aliyejulikana kwa jina la Lushiku Tenganija Sono Msukuma aliyekuwa na
Umri wa Miaka 59 wa kitongoji cha Senga kata ya Bugando Mkoani Geita
ameuawa na mwili kuonekana muda wa Saa moja asubuhi ukiwa kwenye
barabara ya mtaa umbali wa mita kama mia tatu kutoka nyumbani alipokuwa
akiishi Marehemu pamoja na wajukuu zake watatu.
Maremu
amekatwa shingo kabisa na kutenganishwa na Mwili, mkono wa kushoto na
kulia pamoja na bega la kulia. Afisa Mtendaji wa Kijiji hicho Bwana Joel
Saanane (42) amethibitisha kutokea kwa Tukio hilo na kudai kuwa msako
mkali unaendelea dhidi ya wauaji hao.
Na Geita yetu Blog.