MKURUGENZI wa zamani wa Shirika la Umeme nchini, (Tanesco) William
Geofrey Mhando na mamsap wake, Eva Stephem Mhando, na maofisa wengine
watatu wa shirika hilo, France Lucas Mcharange, Sophia Athanas Misidai
na Naftali Luhwano Kisinga, leo wamepandishwa kizimbani Mahakama ya
Kisutu jijini Dar es Salaam kwa kosa la kuhujumu uchumi na kuiingizia
serikali hasara ya zaidi ya shilingi milioni 884,550,000.
Katika kesi hiyo iliyosomwa na Wakili wa Serikali, Leonard Swai,
mbele ya Hakimu Frank Mushi, wakili huyo alisema Mhando akiwa Mkurugenzi
Mtendaji wa Tanesco anatuhumiwa kumpa tenda mamsap wake ya kusambaza
vifaa vya stationery vyenye thamani ya shilingi milioni 884,550,000/ kwa
shirika hilo kinyume na taratibu.
(PICHA : RICHARD BUKOS NA ISSA MNALLY/GPL)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)