Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akifurahia
jambo wakati akitoa hotuba yake katika mkutano wa Wadau wa Ukanda wa
kati(alignment meeting on central corridor), alioufungua leo mchana
katika ukumbi wa Mwl. Julius Nyerere. Mkutano huo wa wadau ni sehemu ya
utekelezaji wa maamuzi ya Mkutano wa Jukwaa la Kiuchumi Duniani (World
Economic Forum) iliofanyika Davos Uswiss Mwezi Januari 2014.
Waziri
wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe, akitoa hotuba kabla ya
kumkaribisha kufungua mkutano wadau wa Ukanda wa kati (alignment meeting
on central corridor), uliofanyika leo mchana katika ukumbi wa Mwl.
Julius Nyerere. Kulia kwa Waziri Mwakyembe ni Mkurugenzi wa Jukwa la
Kiuchumi Duniani kwa upande wa Afrika, Bi. Elsie Kanza.
Sehemu
ya washiriki wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt.
Shaaban Mwinjaka wakati akiwasilisha mada katika mkutano wa wadau wa
Ukanda wa kati (alignment meeting on central corridor), uliofanyika leo
mchana katika ukumbi wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akimwambia
jambo Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Bw. Richard Sezibera,
wakati wa mkutano wa Wadau wa Ukanda wa kati (ALIGNMENT MEETING ON
CENTRAL CORRIDOR), uliofanyika leo mchana katika ukumbi wa Mwl. Julius
Nyerere. Mkutano huo wa wadau ni sehemu ya utekelezaji wa maamuzi ya
Mkutano wa Jukwaa la Kiuchumi Duniani(World Economic Forum) iliofanyika
Davos Uswis Mwezi Januari 2014.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka akiwasilisha mada ya
fursa ya uwekezaji katika Ukanda wa kati, katika mkutano uliowakutanisha
Wadau wa Ukanda wa kati(alignment meeting on central corridor),
uliofanyika leo mchana katika ukumbi wa Mwl. Julius Nyerere,jijini Dar
es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete (wa sita kutoka
kulia), akiwa katika picha ya pamoja na Wahisani wa maendeleo, na
waadau wa mkutano wa Wadau wa Ukanda wa kati wa(alignment meeting on
central corridor), uliofanyika leo mchana katika ukumbi wa Mwl. Julius
Nyerere jijini Dar es Salaam. Mkutano huo wa wadau ni sehemu ya
utekelezaji wa maamuzi ya Mkutano wa Jukwaa la Kiuchumi Duniani (World
Economic Forum) iliofanyika Davos Uswiss Mwezi Januari 2014, ambao
ulichagua Ukanda wa kati kuwa mradi wa majaribio ya kuwezesha uwekezaji
kwa njia ya ubia(PPP).(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi)