Mwanamke wa miaka
20 amekunywa sumu mpaka kufa baada ya kufumaniwa na mumewe akifanya
mapenzi na mjomba wa mume huyo jumapili iliyopita. Msemaji wa jeshi la
polisi wa Mashonaland inspekta msaidizi Nobert Muzondo amekiri kutokea
tukio hilo.Alimtambua marehemu kuwa ni Molyn Mudonhi wa mtaa wa 4232 barabara ya Sangano, Rusike Park. Inspekta
anasema uchunguzi wa tukio hilo unaendela. Anasema siku ya tukio mnamo
saa moja jioni, mume wa Mudonhi, Regway Matimaka alirudi nyumbani na
kumkuta mke wake akifanya mapenzi na mjomba wake.
Ugomvi
ulizuka kati ya Matimaka na mjomba wake hali iliyosababisha Mudonhi
kunywa sumu. Baada ya kugundua kuwa Mudonhi amekunywa sumu, Matimaka na
mjomba wake walishirikiana kumkimbiza MKE WAO katika hospitali ya
Marondera ambako alifariki dunia baada ya kuchekiwa na daktari.
Mwili
wake ulipelekwa kwenye chumba cha maiti ili kufanya uchunguzi zaidi ya
ki-daktari. Inspekta Muzondo alisema watu wanabidi watambue umuhimu wa
maisha na mara zote watafute ushauri kutoka kwa wataalamu wa
kisaikolojia.
Home » Uncategories » MKE ANYWA SUMU NA KUFA BAADA YA KUFUMANIWA NA MUME AKIFANYA MAPENZI NA MJOMBA WA MUMEWE
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
1 comments:
weka pic nzima