Katika
jambo ambalo limevuta hisia za wanafunzi wengi na walimu wa Chuo cha
Mwenge ni Tukio lililotokea leo Majira ya Jioni hii katika Chuo cha
Mwenge kilichopo Moshi.
Kwa Mujibu wa mzazi wa watoto wanaotuhumiwa kubakwa aitwaye Redenta
Boniface Tarimo alieleza tukio zima kuwa siku ya ijumaa majira ya Jioni
Binti yake aitwaye Modesta Boniface Tarimo mwenye umri wa miaka 15 na ni
mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari Maki Sekondari
iliyoko Olele huko Marangu Kitowo alitoweka nyumbani Huko Marangu Kitowo
akiwa na mwenzake aliyetambulika kwa jina la Kresta A. Mroso mwenye
umri wa Miaka kumi na sita na hawakuweza kuonekana mpaka jumapili jioni.
Baada ya kuonekana ndipo walipobanwa na kusema walikua Moshi mjini kwa
Mwanaume ambaye alikua ni mwalimu wao shuleni na anasoma chuo cha
Mwenge.
Afisa wa Polisi anayeshughulikia Dawati la Jinsia na Watoto Afande
Kasusura akiwa amemkamata Mtuhumiwa mmoja aitwaye Majaliwa nje ya chuo
cha Mwenge.
Baada ya maelezo ya watoto ha Jeshi la polisi kwa kushirikiana na
Wazazi wa watoto hao ndipo walipofika katika chuo hicho na kuweza
kuwatia mbaroni wanafunzi hao Ndugu Sebastian Mashauza Mwenyeji wa
Kigoma na ni mwanafunzi wa Mwaka wa kwanza na Mwenzake alitambulika kwa
jina moja la Majaliwa Mwenyeji wa Kigoma na ni mwanafunzi wa mwaka wa
kwanza katika chuo hicho.
Mtuhumiwa akioneshwa watoto alioshiriki kuwabaka waliopo ndani ya Gari kabla ya kwenda kuonesha mwenzake alipo.
Modesta akizungumza na muandishi wetu alisema Anamtambua Sebastian
Mashauza kama mwalimu wake alikuja shuleni kwao akawa anawafundisha somo
la Kiswahili, Baada ya mwezi mmoja aliondoka wakawa wanawasiliana kwa
njia ya simu na siku ya ijumaa ndio mwalimu huyo akamtumia shilingi elfu
kumi kwa njia ya M Pesa ili aje mjini na akamwambia aje na mwenzake
ndipo alipomuomba Rafiki yake Kresta amsindikize na walipofika ulipofika
usiku Mwalimu huyo akamshawishi walale ndipo mwalimu huyo alipomwambia
Kresta alale na Rafiki yake aitwaye Majaliwa. Mwanafunzi huyo alizidi
kusema kuwa walipotaka kuondoka siku inayofuata hawakupewa nauli ndipo
ikapelekea walale tena mpaka siku ya jumapili walipopewa nauli na
kuondoka kurudi nyumbani.
Afande Kasusura akimpeleka Mtuhumiwa kuonesha mwenzake alipo
Hata hivyo uchunguzi wa awali umebaini kuwa Sebastian Mashauza
alifundisha katika shule ya Maki sekondari anayosoma Modesta na alikua
kama mwalimu wa field hapo kwa kipindi cha mwezi mmoja. Kwa sasa
watuhumiwa wako Kituo cha Polisi cha Marangu tayari kwa kusubiri
Utaratibu wa kisheria kukamilika kabla ya kupelekwa Mahakamani.
Majaliwa akitolewa ndani ya nyumba wanayoishi na ndio nyumba iliyotumika kuwabaka watoto hao baada ya mwenzake kupatikana
Mtuhumiwa namba moja Sebastian Mashauza mwalimu aliyewarubuni wanafunzi wake akiwa chini ya ulinzi mkali.
1 comments:
Hawa wajinga sana; na ndio wanategemewa kuwa walimu wakati hata vichwa vyao havifanyi kazi sawasawa. Kwani inahitaji elimu ya chuo kikuu kujua kuwa ukimtorosha mtoto mdogo na kulala nae usiku mzima ni kosa la jinai? Hawa wanastahili adhabu kali sana.