Mwanadada aliyetambulika kwa jina la Asha baada ya kufumaniwa akisindikizwa na ngoma.
Tukio hilo lililofunga mtaa lilijiri asubuhi ya saa 3:14 Jumatatu
iliyopita eneo maarufu kwa jina la Sultani baada ya mwanaume huyo
kutonywa kuwa, mke wake alikuwa amelala kwa rafiki yake kipenzi,
Abdallah Elias.Baadhi ya wananchi waliobahatika kuwasili katika eneo la tukio walishuhudia mwenye mali akiwashushia kichapo kikali ‘wasaliti’ hao ambapo vurugu zikapamba moto.
Kufuatia hali hiyo, viongozi wa serikali ya mtaa huo waliamua kutoa taarifa kwa Kamanda Mkuu wa Ulinzi wa Jadi Kata ya Mbuyuni, Aidan Mtimbo ambaye alifika eneo la tukio na vijana wake na kuwasomba watuhumiwa hao msobemsobe huku wakisindikizwa na ngoma hiyo hadi Kituo cha Polisi Kata ya Mbuyuni.
Vijana wakipiga ngoma wakati wa fumanizi la Asha.
Katika hali ya kushangza, nje ya kituo hicho cha polisi baadhi ya
wananchi waliokuwa na hasira walishinikiza watuhumiwa watolewe nje
wawafanyie kitumbaya huku baadhi yao wakikipopoa mawe kituo hicho
kilichokuwa na askari mmoja aliyevaa nguo za kiraia.Baada ya vurugu hizo, afande huyo alipiga simu kituo kikuu cha polisi kuomba msaada ambapo askari wa pikipiki walifika na kuwakodia teksi watuhumiwa hadi kituoni.
Mwandishi wetu alifanikiwa kuwahoji wahusika wote watatu ambapo mume wa mwanamke huyo ndiye aliyekuwa wa kwanza kuzungumza kama ifuatavyo:
“Huyu mwanamke ni malaya sana, kwanza nimemtoa kwao Matombo (Morogoro) akiwa na watoto wawili na kila mmoja na baba yake.
“Mimi sikujali hilo, ukipenda bonga penda na ua lake. Miezi mitatu iliyopita aliniambia ana ujauzito wangu, taarifa hizo zilinifurahisha sana. Cha ajabu juzi akaniambia ametoa mimba yangu, nilipomuuliza kwa nini, akasema kwa ujeuri eti hayupo tayari kuzaa na mimi kwa sasa.
“Nilichukua uamuzi wa kumrudisha kwao, jana usiku napokea taarifa kuwa yuko nyumbani kwa rafiki yangu kipenzi, Abdallah Elias.
Polisi baada ya kutinga eneo la tukio kuwanusuru watuhumiwa.
“Ndiyo asubuhi nikakodi ngoma na kwenda, niliwakuta wamelala kitandani.”Kwa upande wake Elias alipotakiwa kuzungumzia tukio hilo, alisema:
“Huyu mwanamke ni mbaya sana, ametuchanganya mimi na rafiki yangu Dullah, yeye kaja kwangu jana Jumapili akaniambia amefukuzwa na mumewe hivyo anaomba alale kwangu kesho yaani leo aende kwao Matombo kumbe alisharudishwa kwao toka juzi.”
Naye mwanamke huyo alipohojiwa na paparazi wetu alikuwa na haya ya kusema:
“Huyu mwanaume (Ramadhan) hajanioa, kila siku nikimwambia twende kwa wazazi wangu ananipiga danadana. Ni kweli nimetoa mimba yake, siko tayari kuzaa naye mtoto nje ya ndoa. Huyu Elias, yeye alionesha nia ya kunioa.”
Mume wa Asha, Ramadhan Ally.
Diwani wa Kata ya Mbuyuni, Samuel Msuya amethibitisha kutokea kwa
fumanizi hilo kwenye mtaa wake lakini aliwatupia lawama polisi wa
pikipiki kwa kupuuza uongozi wa juu wa kata hiyo ambao kwa kushirikiana
na walinzi wa jadi walifanikiwa kuwalinda watuhumiwa wao na kufika
salama kwenye kituo cha polisi.