Wananchi wakiangalia lori hilo la mafuta baada ya kuteketea kwa moto baada ya ajali.
Mabaki ya lori hilo bada ya kuteketea.
Baadhi ya wasafiri wakitazama lori lililoungua jioni hii.
Bonde la milima Sekenke linavyoonekana na baadhi ya miti ikiwa imeungua.
Hii ni njia katika milima ya Sekenke.
Haya ni mabaki ya mwili wa mmoja ya watu waliokuwa kwenye lori hilo.
Moto ukimalizikia kwa mbali kama inavyoonekana.
LORI la mafuta limeanguka jioni hii katika eneo la milima ya sekenke mkoani Singida na kuua watu wanne papohapo.
Chanzo cha
ajali hiyo ni kufeli breki lori hilo kukamata moto wakati lilipokuwa
linashuka milima hiyo. Shuhuda wa ajali hiyo, bwana Julius Chacha
alipoongea na Dj Sek Blog amesema kuwa lori hilo lilipoacha njia
lilipinduka na kuingia bondeni na kushika moto.
Akiendelea
kuongea, shuhuda huyo alisema walishindwa kutoa msaada wowote kwa kuwa
moto uliposhika ulikuwa mkubwa na hawakuwa na vifaa vya kuokolea. Watu
wanne wamekufa papohapo kutokana na ajali hiyo. Polisi walikuwa bado
hawajafika eneoo la tukio mpaka tunaondoka eneo la tukio.
(Picha na DJ Sek Blog)