WAKATI mchakato wa Bunge la Katiba ukianza leo mjini Dodoma, ishu
hiyo imemtia kwenye tope Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF),
Simon Mwakifwamba baada ya kukwaa skendo ya ‘kutoka’ na mwigizaji
Yobnesh Yusuph ‘Batuli’ walipotimba mkoani humo.
“Akina Monalisa (Yvone-Cherry Ngatikwa) walistahili kwa ukongwe wao kwenye fani, sasa Batuli aliingiaje? Akili za kuambiwa changanya na zako,” alisema msanii huyo.
Akizungumzia skendo hiyo, Mwakifwamba alidai kuwa ameshasingiziwa vitu vingi hivyo anajua nyuma yake kuna kundi linalomchafua kila kukicha lakini ukweli ni kwamba hakumteua Batuli kwa lengo hilo.
“Sasa kama nimemteua kwa sababu hiyo, je, akina Monalisa nao niliwateua kwa kigezo hicho?” alihoji Mwakifwamba huku akikiri kuwa ameshaisikia sana skendo hiyo.
Yobnesh Yusuph ‘Batuli’.
Kwa mujibu wa staa wa filamu ambaye aliachwa katika safari hiyo ya
kwenda kuhamasisha sanaa itambuliwe kwenye mchakato wa katiba mpya,
Mwakifwamba alimteua Batuli ili akajiachie naye Dodoma kwa sababu hakuwa
na vigezo.“Akina Monalisa (Yvone-Cherry Ngatikwa) walistahili kwa ukongwe wao kwenye fani, sasa Batuli aliingiaje? Akili za kuambiwa changanya na zako,” alisema msanii huyo.
Akizungumzia skendo hiyo, Mwakifwamba alidai kuwa ameshasingiziwa vitu vingi hivyo anajua nyuma yake kuna kundi linalomchafua kila kukicha lakini ukweli ni kwamba hakumteua Batuli kwa lengo hilo.
“Sasa kama nimemteua kwa sababu hiyo, je, akina Monalisa nao niliwateua kwa kigezo hicho?” alihoji Mwakifwamba huku akikiri kuwa ameshaisikia sana skendo hiyo.
Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Simon Mwakifwamba.
Kwa upande wake Batuli alifunguka: “Si kweli bwana, wameshatuzushia
mambo kibao. Mara kuna fedha tumekula, mara sijui nini…sasa naona
wamekuja na hili la mapenzi. Wabongo tuache majungu.
Katika safari ya Dodoma, mbali na Monalisa, wawili hao waliambatana
na wasanii wengine wa tasnia mbalimbali wakiwemo Dude, John Kitime,
P-Funk Majani na Abdul Salvador ambapo ndani ya bunge hilo
linalotarajiwa kutikisa, wanawakilishwa na Paul Mtendah.