Kuna vurugu kati ya wakulima na wafugaji, wakulima wameamua kufunga barabara ( Morogoro - Iringa) hapa mbele ya kidogo ya Mindu Melela wanataka kusikilizwa na kutatuliwa kutatua mgogoro wao na wafugaji. Hakuna magari yayokwenda wala yanayorudi. RPC na FFU wamefika lakini hali si shwari wananchi wanamtaka mkuu wa mkoa hawamtaki mkuu wa wilaya.

HALI ya usalama kwa magari ya abiria na magari ya mizigo wanaotumia barabara hiyo ni tete kwa sasa.

Foleni ya magari ni kubwa maana hakuna gari iliyoruhusiwa kupita tangu majira ya saa 3 picha zitakujia punde.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...