Home »
Uncategories »
ASKARI MOSES ALPHAGE ALAMBA MILIONI 2 KWA BIDII YA KAZINI
ASKARI MOSES ALPHAGE ALAMBA MILIONI 2 KWA BIDII YA KAZINI
Unknown
3:47 PM
Mfanyaakazi
wa Idara ya Masoko wa Kampuni ya Vodacom Albert Maneno (wa tatu
kushoto) akiongea kabla ya kukabidhi Sh. milioni 2 kwa askari wa kikosi
cha Usalama Barabarani Moses Alphage (wa kwanza kushoto) aliyeibuka
kidedea katika programu ya kuibua hamasa ya kazi kwa askari hao jijini
Dar es salaam iliyoendeshwa na kituo cha Redio Clouds FM. Fedha hizo
zimetolewa na wafanyakazi wa Vodacom pamoja na wananchi mbalimbali
walioguswa na programu hiyo. Wa kwanza kulia ni Kamanda wa Polisi Kanda
Maalum ya Dar es salaam Kamishna Suleiman Kova.
Kamanda
wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Kamishna Suleiman Kova,
akipokea sh. milioni 2 kutoka kwa mfanyakazi wa Vodacom Tanzania Albert
Maneno zilizochangwa na wafanyakazi wa Vodacom na wananchi mbalimbali
kwa ajili ya askari wa kikosi cha usalama barabarani Moses Alphage
aliyeibuka kidedea katika programu ya kuibua hamasa ya kazi kwa askari
hao jijini Dar es salaam iliyoendeshwa na kituo cha Redio Clouds FM.
Kamanda
wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova akimkabidhi
Askari wa usalama barabarani, Moses Alphage fedha taslimu Sh. milioni 2
zilizochangwa na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania na wasikilizaji wa
kituo cha Redio Clouds FM kupitia programu ya kuhamasisha na kupongeza
utendaji kazi wa askari wa usalama barabarani jijini Dar es salaam
iliyonedeshwa na kituo hicho cha Redio. Alphage huongoza magari katika
daraja la Mlalakuwa, Kawe.
Askari wa usalama barabarani, Moses Alphage, akiondoka zake kwa mwendo
wa kikakamavu mara baada ya kukabidhiwa cheti na pesa taslimu kiasi cha
zaidi ya shilingi milioni 2 na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es
salaam Suleiman Kova (hayupo pichani).
Kamanda
wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova (wa tatu toka
kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Askari wa usalama barabarani,
Moses Alphage (wa pili kushoto) aliyeibuka kidedea kwenye programu ya
kuhamasisha na kupongeza utendaji kazi wa askari wa usalama barabarani
jijini Dar es salaam iliyonedeshwa na kituo hicho cha Redio na
kujishindia Sh milioni 2. Wa kwanza kushoto ni Mfanyakazi wa Vodacom
Tanzania Albert Maneno na kulia ni mtangazaji wa Clouds Said Mohamed
maarufu Bonge.