Doto Omari kushoto aliyeunguzwa na moto wa ajabu sehemu za siri.
Na Chande Abdallah
KATIKA
tukio linalohusishwa na ushirikina, mwanamke mmoja aliyejulikana kwa
jina la Doto Omari (30, pichani) ameunguzwa na moto wa ajabu sehemu zake
za siri.
Moja ya jeraha alilolipata.
Tukio
hilo la aina yake lilitokea alfajiri ya Machi 16 mwaka huu,
Mwananyamala – Kichangani, Dar, wakati mwanamke huyo alipokwenda chooni
kujisaidia.
Akizungumza
na waandishi wetu, Doto alisema alipoanza kujisaidia, alishangaa kuona
moto mkubwa ukitokea ndani ya shimo la choo na kumuunguza sehemu zake za
siri, jambo lililomfanya apige kelele kuomba msaada.
“Yaani
ule moto ulikuwa mkubwa halafu wa kijani huku ukiwa na muungurumo wa
ajabu. Mimi nilishangaa kuuona ukinifuata na kuniunguza,” alisema.
Kaka wa
mwanamke huyo aliyejitambulisha kwa jina la Adam, alisema aliposikia
kelele za moto, alikimbilia maji akijua ni wa kawaida.
“Mpaka
sasa tumechanganyikiwa sana, hilo siyo tukio la kwanza, yako mengi,
nilishawahi kumuona mtu wa ajabu kainama kwenye mlango wa kuingilia
chooni halafu kufumba na kufumbua akapotea, hii nyumba siyo kabisa.
“Wengi
ukiwaambia jambo hili huona kama hadithi, lakini matukio ya aina hii
hapa Kichangani ni jambo la kawaida sema watu wanaogopa kusema,” alisema
Adam.
Naye wifi
yake Doto aliyeomba hifadhi ya jina lake, alisema aliona moshi mweusi
ukitokea chooni huku kukiwa na harufu ya kama kitu kinachoungua, ingawa
hakuuona moto zaidi ya kumuona wifiye akigaragara chini akidai kuungua.
Hadi
waandishi wetu wanaondoka eneo la tukio, ndugu hao walikuwa wakijiandaa
kumpeleka Doto kwa mganga wa kienyeji maeneo ya Lugoba, Chalinze kwa
matibabu.SOURCE GPL