Na Waandishi Wetu
KAMANDA wa kampuni moja ya ulinzi ya jijini Dar es Salaam (jina
tunalo), Japhet Misana ambaye pia ni mkuu wa kitengo cha mafunzo cha
kampuni hiyo, Alhamisi iliyopita wakati Wakristo wakiwa kwenye hekaheka
za Sikukuu ya Pasaka, alinaswa gesti akiwa na askari wake ambaye ni mke
wa mtu.
Kamanda akiwa katika hali ya sintofahamu baada ya kunaswa akiwa na askari wake ambaye ni mke wa mtu.
Kamanda huyo na askari wake (jina tunalo) walijichimbia kwenye gesti hiyo iliyopo Tabata Matumbi, Dar kwenye chumba namba 6.
Kamanda wa kampuni ya ulinzi, Japhet Misana akivaa baada ya kunaswa akiwa na mke wa mtu.
Ilidaiwa na chanzo chetu kuwa, kamanda huyo alianza kutokwa na ‘mate’
ya matamanio kwa askari wake huyo tangu alipofika kwenye kampuni hiyo
kuomba kazi.
...Akiwa chini ya ulinzi wa polisi.
Chanzo hicho kiliendelea kudai kuwa, askari huyo alipewa kazi kwa
sharti la kutoa ‘burudani’ kwa kamanda huyo lakini baada ya kufanikiwa
kupata ajira alianza kumpiga danadana mkubwa wake huyo kuhusu suala la
‘majamboz’ kama walivyokubaliana.
“Wakati
danadana zikiendelea wapambe walimng’ata sikio mwenye mali kwa
kumwambia kwamba asiwe ‘babu jinga’ kwani mali zake zinakaribia kuliwa
na wapenda vinono,” kilisema chanzo.
Taarifa hizo, kwa mujibu wa chanzo, zilimshtua sana mwanaume huyo
ambaye alianza kumwekea mtego mkewe pamoja na bosi wake kwa kumkabidhi
kazi hiyo mdogo wake kuwa ‘shushu’.
Siku ya Alhamisi Kuu ambayo kimvua kilisumbua karibu jijini zima la
Dar sanjari na kibaridi, shushu huyo alimsikia shemeji yake akizungumza
kwenye simu na mtu mmoja aliyehisiwa kuwa ndiye kamanda wakiahidia
kukutana kwenye gesti hiyo.
Shushushu huyo haraka alipiga simu kwenye chumba cha Oparesheni
Fichua Maovu (OFM) na kuwaeleza mchezo mzima.Baada ya kupata taarifa
hizo bila kuzubaa, makamanda wa OFM walitumia dakika zisizozidi 10
kutoka makao makuu ya ofisi zao zilizopo Bamaga-Mwenge jijini Dar na
kuwasili eneo la tukio.
OFM na shushu huyo waliwaona wawili hao wakiongozana na kupiga kona
kadhaa kisha wakaingia kwenye gesti hiyo na kujichimbia kwenye chumba
namba sita.Wawili hao wakiwa chumbani makachero wa OFM waliwasiliana na
askari Polisi wa Kituo cha Tabata ambao nao waliwasili bila kuchelewa.
Walipofika waliingia ndani ya gesti hiyo na kumtaka mhudumu,
walijitambulisha na kumweleza kilichowaleta pale ambapo mfanyakazi huyo
wa mapokezi alikwenda kuwagongea wateja wake bila kuwaeleza kama
arobaini yao ilitimia.
Kwa mujibu wa mpelelezi aliyetumwa na mume wa mwanamke huyo, mwanamke
ndiye aliyefungua mlango akiwa na taulo huku kamanda wake akiwa
kitandani.
Shushushu huyo aliongeza kuwa, baada ya kushuhudia tukio hilo
alipandwa na jazba na kutaka kuwapa kipondo lakini polisi walimzuia na
kumtia pingu kamanda huyo hadi kituo cha polisi.
Kamanda huyo na askari wake walifikishwa
kituoni hapo na kuchukuliwa maelezo ambapo mwanamke huyo aliweka wazi
tangu bosi wake huyo alipompa ajira kwa sharti la kumpa burudani na
mengineyo.
Kamanda Misana alifunguliwa kesi ya kudai rushwa ya ngono kwenye jalada lenye namba TBT/RB/2280/2014 na kutupwa rumande.
Kamanda Misana alifunguliwa kesi ya kudai rushwa ya ngono kwenye jalada lenye namba TBT/RB/2280/2014 na kutupwa rumande.
Stori: Richard Bukos, Makongoro Ogong’, Haruni Sanchawa na Issa Mnally.