Kaimu Kamanda wa polisi wa mkoa huo, Joseph Konyo ambaye ni Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai akitoa taarifa. |
Matukio hayo ambayo niya
kipindi cha kuanzia Januari hadi Juni mwaka huu kutokana na wizi huo uliofanywa
na makundi ya watu mbalimbali yanaujihusisha na utapeli, wananchi hao ambao
baadhi ni watu maarufu Jijini hapa, ‘wamelizwa’ kiasi cha shilingi
Milioni 309 kwa kipindi hicho.
Kaimu Kamanda wa polisi
wa mkoa huo, Joseph Konyo ambaye ni Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya
Jinai Mkoani hapa akitoa taarifa za matukio hayo jana kwa waandishi wa habari
ofisini kwake, alisema kuwa ,baadhi ya matapeli waliokamatwa wameisha fikishwa
mahakamani huku wengine wakiendelea kusakwa.
Katika tukio la hivi
karibuni mwezi uliopita, mwananchi mmoja maarufu jijini Mwanza (hakutajwa)
mkazi wa Kiseke wilayani Ilemela, alinaswa na mtego wa matapeli hao na kujikuta
akiuziwa kilo kumi za unga wa sembe ambao ulikuwa umehifadhiwa kwenye begi
ikidaiwa ni madini ya Rubi (Green Tourmaline)
“Huyu alilazimika kuuza
nyumba yake jijini Mwanza na kwenda na matapeli hao hadi Morogoro ambapo
alionyeshwa madini hayo na kutoa pesa na kisha kufungiwa kwenye begi bila
kutakiwa kulifungua hadi atakapofika Mwanza na kukaa siku saba vinginevyo
atakiuka masharti na kukuta majini.” Alielza Konyo.
Alieleza kuwa , baada ya
siku tatu kupita, mkazi huyo aliwapigia simu wauzaji akitaka kufungua lakini
walimzuia kuwa asubiri hadi watakapomueleza, akilazimisha atakuta majini, hali
iliyomfanya akimbilie polisi ili kuomba msaada wa kulifungua na ndipo
ilipobainika kulikuwa na unga wa sembe na si madini.
“Huwezi kuamini na
ukimuona huto amini kama angesitahili kuibiwa kiurahisi (Kutapeliwa) namuna
huyo ni mtu anaheshimika hata kimuonekano wake na kibaya zaidi alimpa talaka
kwanza mkewe ndiyo akuza nyumba yake ili kupata fedha za kupata madini hayo,
sasa mke kamkosa, nyumba imeenda, fedha na madini kavikosa.” Alisema.
Tukio jingine, ni
mkulima mmoja aliuza nyumba yake kwa thamani ya sh milioni 7 na fedha hizo
kuuziwa chupa ya dawa feki ya kuhifadhia mazao ambayo alidanyanywa kuwa
angeweza kuiuza kwa wakulima wenzake kwa sh milioni 100 na kwamba dawa hiyo
inatafutwa na wazungu na inapatikana katika Chuo cha Utafiti Ukiriguru pekee
hivyo kwake atweza kuvuna kiasi hicho.
“Mwingine aliuziwa chupa
tatu za chuma (Mitungi midogo) zilizojazwa kokoto na cimenti (ndani) kwa
tahamani ya shilingi milioni 26, akidanganywa kuwa ni za asidi (mercury) ya
kuoshea dhahabu na mwingine akadanganywa asiweke fedha benki
wamuuzie dhahabu, akauziwa gorori za baiskeli kwa shilingi milioni 6 baada ya
kuonyeshwa vipande vya kufuli vilivyosagwa na kung’aa kama dhahabu.” Alisema
Konyo.
Kamanda huyo alieleza
kuwa, katika tukio jingine, mwananchi mmoja aliyeuza nyumba yake shilingi
milioni 200, alidanganywa kuwa wanaweza kuzarisha fedha zake mara mbili na
kuziweka kwenye boksi la mganga mmoja ili ziwe sh milioni 400, matokeo yake
alibiwa, watuhumiwa walikamatwa kesi iko mahakamani.
Akihitimisha matukio
hayo la mwisho, alisema kuwa mwanamke mmoja mfanyabiashara alijikuta akibakwa,
kulawitiwa na kuibwa pesa (hazikutajwa) baada ya kufanya mazungumzo katika
chumba cha Hoteli moja jijini hapa na kujikuta akinyweshwa dawa za kulevya na
watu hao waliojitambulisha kwake kuwa ni wafanyabiashara kutoka Miji mikubwa
Kaimu kamanda huyo
ametoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Mwanza, alisema matapeli hao wakati
mwingine wanatumia majina ya viongozi wa ngazi za juu mkoa na taifa hivyo wawe
makini kubaini mbinu zinazotumiwa na ikiwezekana kutoa taarifa mapema kabla ya
kutoa fedha kwani mbinu nyingine ni za kizamani, zinahitaji akili ya utambuzi
wa ukweli na uongo.
“Ebu sasa viongozi na
wafanyabiashara ambao kila kukicha matapeli wanapanga njama za kuwadanganya kwa
lengo la kuwaibia na kuwatapeli wafanye mawasiliano kwanza emdapo matapeli hao
watawafika na kutumia majina ya viongozi wengine wakiwemo wa vyombo vya ulinzi
na usalama kabla ya kutekeleza kile walichoombwa ikiwemo kutoa taarifa kwa
Jeshi la Polisi ili kuwakamata” alisisitiza
KWA HISANI YA G SENGO BLOG