Jengo la Westgate nchini Kenya.
Wanaume wanne wamefikishwa mahakamani nchini Kenya baada ya
kuhusishwa na shambulizi la kigaidi lililofanyika dhidi ya jengo la
Westgate nchini Kenya mwezi Septemba.Wanne hao wote walikanusha
mashitaka hayo ikiwemo kosa la kuingia nchini bila vibali halali pamoja
na kumiliki stakabadhi bandia za kujitambulisha. Mahakama imeamuru
wawekwe rumande. Kundi la kigaidi la Somalia, Al Shabaab lilikiri
kufanya shambulizi hilo la kigaidi ambapo zaidi ya watu sitini waliuawa.
Wanne hao walishitakiwa kwa kosa la kuhusika na shambulizi hilo la kigaidi ingawa hakuna hata mmoja alikuwemo ndani ya Jengo la Westgate wakati wa shambulizi hilo.
Wanne hao raia wa Somalia ni Mohammed Ahmed Abdi, Liban Abdullah, Adan Adan na Hussein Hassan. Washukiwa hao ambao hawakuwa na mawakili walizuiliwa rumande kwa wiki moja baada ya kiongozi wa mashitaka kuomba muda zaidi kufanya uchunguzi.

CHANZO BBC SWAHILI.