Watu
watatu wakazi wa Mwananyamala Jijini Dar Es Salaam wamejeruhiwa katika
tukio lililohusisha risasi za moto linalodaiwa kufanywa na polisi baada
ya kukutwa wakikesha kwenye ngoma maarufu za Kigodoro, ambazo tayari
zimekwishapigwa marufuku na jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es
Salaam.Tukio hilo lilitokea majira ya saa kumi na nusu jioni katika eneo la shule ya msingi kisiwani ambapo mmoja
wa majeruhi hao tayari amekwisahruhusiwa kurudi nyumbani na mwingine
akiendelea na matibabu kwenye hospitali ya Mwananyamala.
Wakiwa
kwenye ngoma hiyo maarufu Jijini Dar es Salaam ya Kigodoro, eneo la
Kisiwani mwananyamala, mara gahfala polisi walivamia eneo hilo, na
kusimamisha shughuli nzima kwa madai ya kucheza wakiwa hawana nguo,
jambo ambalo ni kinyume na maadili.
Akizungumza
kwa njia ya simu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa kipolisi Kinondoni
Kamishna msaidizi Camillius Wambura anathibitisha kutokea kwa tukio
hilo.