KABAANG! Mume aliyejulikana kwa jina moja la Ngosha, mkazi wa Mabibo jijini Dar, amemfumania rafiki yake aitwaye Jazira akiwa chumbani na mkewe Jack wakiivunja amri ya sita ya Mwenyezi Mungu.
Tukio hilo lilitokea Jumanne iliyopita saa 12 alfajiri ambapo ilidaiwa kuwa Jack alikuwa chumbani na mwanaume huyo ambaye ni mpangaji, wenzake wakipeana maraha.
Picha tofauti juu zikionesha mke wa mtu na mgoni wake katika fumanizi liliotokea.
Imedaiwa kuwa, wawili hao walikuwa wakimtegea Ngosha akitoka kwenda
katika shughuli zake, Jazira alikuwa akizama katika chumba cha rafiki
yake na kufanya mchezo wa kikubwa.
KERO YAVUJISHWA NA MAJIRANI
Wapangaji wenziye na Jack wamedai kuwa, mke huyo wa mtu ambaye ana miezi miwili tangu aolewe kutoka mkoani Tabora, amekuwa kero katika nyumba hiyo kwani amekuwa akipiga kelele za kimahaba nyakati za asubuhi ambapo watu wengi wanakuwa wakielekea kazini.
Wapangaji wenziye na Jack wamedai kuwa, mke huyo wa mtu ambaye ana miezi miwili tangu aolewe kutoka mkoani Tabora, amekuwa kero katika nyumba hiyo kwani amekuwa akipiga kelele za kimahaba nyakati za asubuhi ambapo watu wengi wanakuwa wakielekea kazini.
Hii ni nyumba waliyopanga wafumaniwa hao.
“Hata sisi wanawake tunaoishi nyumba hiyo tuna waume zetu tunawalilia
lakini kinachotusikitisha mwenzetu anamlilia Jazira badala ya mumewe
ambaye anakuwa amekwenda kazini,” alisema mmoja wa wapangaji wa nyumba
hiyo.
Baadhi ya raia waliofika kushuhudia tukio hilo.
MLINZI ABUMBURUA Imeelezwa kuwa, siku hiyo mlinzi wa msikiti alikwenda kumwamsha Ngosha kwenda kusogeza gari lake ili watu wapite na alipofika katika chumba chake, alikuta mlango wa sebuleni ukiwa wazi lakini hakukuwa na mtu, ila chumbani kwake kulisikika redio ikizungumza kwa sauti kubwa.
...Hiki ni chumba ambacho wafumaniwa hao walinaswa wakivunja amri ya sita.
FUMANIZI LASETIWAJirani mmoja aliyedai kuchoshwa na tabia hiyo, alimshauri mlinzi huyo kwenda kusikiliza kwenye dirisha la chumba hicho na waliposikia sauti za kimahaba wakakubaliana wamtonye mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Kanuni, Mabibo aliyetajwa kwa jina la Asha ambaye alifika na kusikia ‘mchezo’ ukiendelea chumbani.
...Na watoto pia walishuhudia tukio hilo la aibu.
Wakati huohuo, Ngosha akapigiwa simu kuja kushuhudia mchezo huo mchafu wa mkewe alioufanyia ndani ya chumba chake.TIMBWILI ZITO LAIBUKA
Mashuhuda wa tukio hilo walisema, alipofika Ngosha nyumbani na kutonywa kilichotokea alipandwa na hasira na kuangusha varangati kwa rafiki yake lakini baadaye akatulizwa, akamtaka Jazira amlipe shilingi milioni 1.2 ili amuachie mke moja kwa moja.
JAZIRA ANA LAKI 2
Jazira alisema hakuwa na kiasi hicho isipokuwa anaweza kulipa shilingi laki mbili tu, jambo lililomfanya Ngosha kuomba msaada wa askari mgambo na kumpeleka mgoni wake Kituo cha Polisi cha Urafiki kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.