1. Paul Pogba-kiungo wa Ufaransa, miaka 21.
Pogba
akiwa bado ana miaka 21 amekuwa jasiri ndani na nje ya uwanja. Wengi
walishangaa kumuona kiungo huyo akipanda kiwango chake kwa kasi
alipoondoka Manchester United na kujiunga na Juventus mwaka 2012 kwa
lengo ka kutafuta namba katika kikosi cha kwanza.
Amekuwa
shujaa wa Claudio Marchisio katika sehemu ya kiungo kwenye ligi ya Seria
A msimu uliopita na aliichezea Ufaransa mechi ya kwanza ya kirafiki ya
kimataifa machi 2013 dhidi ya Georgia.
Mwezi
Julia mwaka huo huo alifanya kazi kubwa kuisaidia timu ya taifa ya
Ufaransa chini ya miaka 20 katika fainali za kombe la dunia, haikuwa
rahisi kwa Ufaransa kwenda kombe la dunia bili kijana huyu mahiri.
Umahiri
wa Pogba amempatia nafasi ya kucheza timu ya taifa na taarifa nzuri ni
kwamba atakuwa huru nchini Brazil kutoa mchango wake kama alivyofanya
nchini Italia. Kuwepo kwa Yohan Cabaye na Blaise Matuidi katika safu ya
kiungo kutamruhusu Pogba kusogea mbele safu ya ushambiliaji.
Frederic
Lipka, ambaye ni mkurugenzi wa kituo kilichomlea Pogba cha Le Havre
kabla ya kwenda England, alisema mwaka 2010 kuwa kijana huyo yuko vizuri
kiufundi kuliko hata Patrick Vieira wakati akiwa na umri kama wake.
Kwasasa tunasubiri kuona alimaanisha nini.
2. Joel Veltman- Beki wa kati wa Uholanzi, miaka 22.
Habari
njema kwa beki huyu wa Ajax ni kwamba; kocha mkuu wa Uholanzi Van Gaal
ameamua kumpa nafasi katika kikosi chake kinachotumia mfumo wa 4-3-3.
Van Gaal
alimpa nafasi ya kuichezea Uholanzi kwa mara ya kwanza katika suluhu ya
bila kufungana na Colombia mwezi novemba mwaka jana.
Veltman
ni mchezaji kijana wa Ajax, lakini hajulikani kirahisi. Namna
anavyocheza na kimiliki mpira, uwezo wa kupiga mashuti na pasi ndefu
kunaonesha kama amekaa muda mrefu katika kikosi hicho. Kiukweli alicheza
mechi yake ya kwanza wiki chache baada ya msimu wa ligi kuu wa
2011-2014 kuanza na kutulia zaidi. Katika msimu mzima amejiimarisha na
kuwa chaguo la kwanza la Ajax.
Siku si
nyingi anaweza kufanya hayo kwa taifa lake, Mfumo wa kulinda kuanzia
safu ya ulinzi unaopendelea Van Gaal unahitaji wachezaji wanaobadilika
na kuweza kuusoma mchezo na kucheza vizuri. Hii kazi yote ni ya Veltman
na anaimudu vizuri.
Pia Van
Gaal anapenda kuona mpira unakwenda mbele. Kwa maana hiyo Veltman
anaonekana ndiye chaguo sahihi kuelekea fainali za kombe la dunia mwaka
huu. Tusubiri kuona beki huyu atafanya nini?.
3. Bernard, Kiungo wa Brazil, miaka 21.
Kwa bei
yake ya paundi milioni 25, Bernard alizikimbiza timu nyingi wakati akiwa
katika klabu yake ya Atletico Mineiro mwaka jana. Lakini Shakhtar
Donetsk walijikaza kisabuni na kuinasa saini ya kiungo huyo majira ya
kiangazi mwaka jana. Walimpokea vizuri na kuikarimu sana familia yake
baada ya kuwasili Ukraine. Licha ya Bernard kuzoea kwa taratibu maisha
ya soka nje ya Marekani kusini, Shakhtar wanaamini jitihada zao za
kumnasa zilizaa matunda.
Bernard
anacheza mpira wa kasi, anapenda kutanua uwanja kulia na kuingia eneo la
namba 10. Mpaka sasa ameanza mechi tatu tu za kimataifa kati ya 10
alizocheza , na anaonekana atatumika pia msimu huu wa kombe la dunia.
Mbali na
wengi kumdharau kwa urefu wake wa futi 5 na inchi 6 na uzito wa kilo 63,
Bernard amekuwa akionesha kiwango cha ajabu. “Shakhtar hawataki
kuniachia kwa sssa.” Alionya katika mahojiano ya karibuni na O Globo
baada ya Asernal na Tottenham kutangaza tena nia ya kumtaka .
Sasa tunasubiri kuona maajabu yake katika fainali za kombe la dunia mwaka huu katika ardhi yake.
4. Mattia Destro –mshambuliaji wa Italia, miaka 23.
Mambo yalienda tofauti kidogo. Destro angeletwa katika ulimwengu wa soka na José Mourinho.
Alikuwa
mfungaji wake wakati Mourinho akiwa Milan. Mshambuliaji huyo alikuwa
katika kikosi kilichotwaa ubingwa wa UEFA, hata kama hakucheza mechi
yoyote.
Baada ya
Mourinho kuondoka, Destro aliuzwa katika klabu ya Genoa, japokuwa
alianza kuongeza kasi ya kiwango chake baada ya kujiunga na Siena mwaka
2011.
Kiwango
chake kiliwavutia zaidi Roma na kumsajili kwa dau zuri-lakini kuingia
kwa kocha Rudi Garcia katika klabu hiyo kumemweka katika kiwango kikubwa
zaidi na kuiteka dunia.
Destro
amekuwa mshambuliaji bora anayesifiwa na kocha wake, huku akimuelezea
kama “mshambuliaji aliyekamilika”. Hakuna utata wa namba kwake. Katikati
ya mwezi aprili mwaka huu alifunga bao lake la 13 katika ligi ya seria
A, huku magoli yake mengi akifunga dakika za mwisho za 85 kwenye michezo
mingi. Kwasasa kwenye ligi kubwa barani Ulaya hakuna mwenye rekodi ya
mabao ya aina hiyo.
Destro
anafunga kila aina ya goli: amekuwa akipiga mashuti ya mbali na karibu.
Anaweza kuwa chaguo la kwanza katika fainali za kombe la dunia, lakini
kiwango chake kitamuokoa kwasababu ana upinzani mkubwa kutoka kwa Pablo
Daniel Osvaldo.
5. William Carvalho , kiungo wa Ureno miaka 21
Sporting
Clube de Portugal ni akademi kubwa kwa soka la vijana, lakini William
Carvalho ni ushahidi kuwa baada ya kituo hicho kuwakuza nyota wakubwa,
Cristiano Ronaldo na Luis Figo, sasa kinamleta nyota huyo mwenye miaka
21 anayeonekana kuwa kiungo bora zaidi wa Ulinzi na amekuwa na kiwango
kikubwa mno katika klabu ya Lisbon baada ya kurudi katika klabu hiyo
akitokea katika mkataba mrefu wa mkopo kwenye klabu ya Cercle Brudgge.
Kujituma
na kuwajibiki wa Carvalho kulimfanya apewe nafasi ya kucheza kwa mara ya
kwanza katika mechi ya “play-off” kuwania kombe la dunia dhidi ya
Sweden mwezi novemba mwaka jana.
Pia
alicheza kwa dakika zote dhidi ya Cameroon mwezi machi mwaka huu katika
mechi ya kimataifa ya kirafiki na kujihakikishia namba katika kikosi cha
kwanza.
Jambo
jema kwa kocha Paulo Bento ni kuwa nyota wa Porto, Fernando, mzaliwa wa
Brazil, tayari amepata kibali cha kuichezea Ureno, lakini kutokea kwa
Carvalho kunaweza kumfanya asimuhitaji tena.
Manchester
United wamekuwa katika mawindo ya kumnasa Carvalho na ada inayotajwa ni
paundi milioni 30. Bento ni kocha mwenye maamuzi magumu, haitashangaza
kuona anamuanzisha Carvalho katika mchezo wa ufunguzi wa kombe la dunia
dhidi ya Ujerumani.
6. Mario Götze-kiungo mshambuliaji wa Ujerumani, miaka 21.
Ni
mchezaji ambaye aliwashitua wengi baada ya kutolewa tangazo mwezi aprili
2013 kuwa anaondoka Borussia Dortmund na kujiunga na wapinzani wao
Bayern Munich. Mashabiki wa Dortmund waliumia sana kwasababu waliamini
nyota huyo kijana angekuwa msaada mkubwa kwa Jurgen Klopp.
Inawezekana
Gotze aliondoka kwa sababu ya presha ya kutaka kuvunja rekodi ya kuwa
mchezaji ghali zaidi kijana kuwahi kutokea nchini Ujerumani akiwa na
miaka 21. Dau la paundi milioni 37 lilikuwa kubwa sana kwake. Mashabiki
walichukizwa na kitendo cha yeye kuondoka, lakini maslahi ndio ilikuwa
sababu .
Gotze ni
mtulivu ndani na nje ya uwanja, na alidhihirisha hilo baada ya kufunga
bao la kuongoza la Bayern Munich aliporejea katika uwanja wake wa Signal
Iduna Park dhidi ya timu yake ya zamani ya Dortmund mwezi novemba mwaka
jana.
Kwenye
mashindano makubwa ya karibuni, Ujerumani wameshindwa kuonesha cheche
kali na mwaka huu wanahitaji `wauaji` wakali, matarajio yao yapo kwa
Gotze mwaka huu. Wanategemea miujiza yake ya soka, uwezo wake wa kupiga
chenga na kasi yake ya `umeme` na uwezo wa kufunga vinawapa matumaini
makubwa sana Ujerumani.
Hii
ilionekana wakati alipofunga bao moja la mwisho katika mechi ya
kimataifa ya kirafiki dhidi ya Chile baada ya kupokea pasi murua kutoka
kwa Mesut Ozil, ikiwa ni bao lake la saba . Wengi wanaamini nyota wa
Asernal, Ozil atakuwa msaada mkubwa kumpikia mambo Gotze ambaye kuanza
kwake katika kikosi cha Bayern Munich msimu uliopita kulimweka matatani
Frank Ribery. Ujerumani wana bahati ya kuwa na mchezaji muhimu kama
yeye. Ngoja tusubiri kuona atafanya nini Brazil mwezi ujao.
7. Aleksandr Kokorin, Mshambuliaji wa Urusi, miaka 23
Huyu ni
kijana mwenye miaka 23 anayekiongoza kizazi cha soka la Urusi kwa sasa.
Ni rafiki wa vyombo vya habari, anashirikiana na anapatikana mara
nyingi-lakini mbali ya hayo hapo juu ana kipaji kikubwa mno cha soka.
Anzhi kwasasa wanafikiria kumuuza kwa paundi milioni 19, lakini
wanamuuza moja kwa moja katika klabu yake ya zamani ya Dinamo Moscow
kabla ya kucheza mechi yake ya kwanza.
Kokorin
ni mchezaji mwenye akili ya mpira, mjanja na amekuwa mmaliziaji mzuri
msimu wa karibuni. Aliifungia Urusi baadhi ya mabao muhimu yaliyowapa
tiketi ya kwenda Brazil (alifunga mabao manne katika mechi saba
alizoanza).
Urusi
chini ya Fabio Capello wapo kundi moja na Ubelgiji, Algeria na Korea
kusini na watapata faida ya kumtumia nyota huyu mwenye kipaji cha juu.
Urusi
wanaamini kuwa nyota huyu atakuwa na ushirikiano mkubwa na mzoefu
Aleksandr Kerzhakov katika safu ya ushambuliaji. Hii ilionekana wazi
katika mechi ya kirafiki ya kimataifa ambayo Urusi ilishinda dhidi ya
Armenia mwezi machi mwaka huu. Hakuna kingine zaidi ya Urusi kusubiri
furaha kutoka kwa kijana huyu.
8. Mateo Kovacic, kiungo wa Croatia, miaka 19
Ili
kudhihirisha kuwa Croatia imebarikiwa kuwa na viungo mafundi kama Luka
Modric Robert Prosinecki na Zvonimir Boban, sasa Mateo Kovacic mwenye
miaka 19 ni ujio mpya katika kikosi cha nchi hiyo na atacheza pamoja na
mafundi wengine.
Inahitaji
ushahidi? anauliza mwalimu wake wa mpira aliyemkuza Niko Kranjcar,
wakati huo huo naye Boban alikiri kuwa kijana huyo atakuwa mzuri zaidi
yake enzi za nyuma.
Kumbuka
Inter walikubali kumnunua kwa dau la paundi milioni 15 kutoka Dinamo
Zagreb januari mwaka 2013. Makocha wote wawili wa timu hizi alizocheza
wamehangaika kupata namba yake halali uwanjani. Kovacic amepewe jezi
namba 10 ya Wesley Sneijder, na hii inatokana na jinsi Inter
wanavyomthamini wa kipaji chake.
Hajaonesha
kiwango kikubwa sana katika taifa lake, lakini kijana huyo aliisaidia
nchi yake kushinda dhidi ya Serbia kuwania kufuzu kombe la dunia
akicheza kama kiungo wa ulinzi, lakini alionesha soka safi kwenye mechi
ya “play-off” na Iceland, ambapo alifunga bao kwa kupiga chenga hatari.
Sasa Brazil inamsubiri.
9. Eden Hazard , kiungo mshambuliaji wa Ubelgiji,miaka 23
Hazard
amekuwa na kiwango cha juu katika klabu ya Chelsea hata zaidi ya
alivyokuwa katika klabu ya Lille kwenye msimu wake wa mwisho. Ameongeza
matumaini makubwa katika nchi yake kuelekea kombe la dunia na inaelezwa
kuwa hayuko peke yake katika kambi ya Ubelji, wapo wachezaji wengi wenye
kiwango kikubwa na morali kama yeye.
Hazard
amekuwa na safari ndefu. Sasa anataka mafanikio zaidi akianza kuitumikia
Ubelgiji kwenye fainali za kombe la dunia kwa mara ya kwanza akiwa na
miaka 23 ikiwa ni miaka karibu mitatu imepita tangu alipoichezea nchi
yake mechi ya kwanza dhidi ya Kazakhstan kuwania kucheza fainali ya Euro
2012.
Kwasasa
hakuna shaka kabisa juu ya kuanza kwake katika kikosi cha Ubelgiji.
Hazard amekuwa akifanya kazi nzuri kutoka winga ya kushoto na katikati,
japokuwa kufunga mabao mawili tu wakati wa kutafuta tiketi ya kufuzu
kombe la dunia kulisababisha akosolewe. Lakini bado amedhihirisha uwezo
wake akiwa na Chelsea ambapo hakuwa na kizuizi tena cha kufunga. Kama
Hazard ataonesha kiwango kama hicho katika kombe la dunia, basi
tunatarajia Ubelgiji iwe tishio.
10. ackson Martinez, mshambuliaji wa Colombia, miaka 27
Hakuna
mtu nchini Colombia asiyetarajia kuona Radamel Falcao anaimarika zaidi
kuelekea kombe la dunia baada ya kupata majeruhi makubwa ya goti, lakini
hata kama atapona, bado atahitaji msaidizi wake.
Mbali ya
Falcao kuhitaji watu wa kumrithi akiwemo nyota wa Hertha Berlin, Adrian
Ramos na Teufilo Gutierrez wa River Plate, Jackson Martinez ndiye mwenye
nafasi kubwa. Akiwa amerithi jezi namba 9 ya Falcao katika klabu ya
Porto, Jackson amefanya makubwa zaidi kama nyota huyo mwenzake wa
kimataifa, akifunga magoli 41 katika mechi 53 alizoanza akiwa na Porto
tangu alipojiunga na klabu hiyo kutokea klabu ya Jaguares mwaka 2012.
Labda
tuseme anatakiwa kuambiwa juu ya kuzingatia wajibu wake wa kimataifa.
Martinez alianza katika mechi nne tu za kuwania kufuzu kombe la dunia na
hakufunga bao lolote. Lakini msimu huu ana njia ndefu baada ya kupewa
hadhi ya kusimama mbele akiwapiku Fredy Guarin na James Rodriguez.
Jackson
amekuwa na umbo zuri na uwezo wake wa kufunga sio siri. Amefunga mabao
muhimu kwa Porto katika mechi za ligi na kimataifa. Nyota huyo mwenye
miaka 27 anaweza kuwa msaada mkubwa kwa Colombia na kurithi mambo ya
Falcao ambaye hatakuwa fiti sana kutokana na majeruhi.
Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Mtandao