KAMATI YA TAIFA YA UONGOZI YA TASAF YAANZA KUKAGUA MIRADI MKOANI RUVUMA

 Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Hassan Bendeyeko akitoa ufafanuzi juu ya utekelezaji wa miradi ya TASAF katika halmashauri za wilaya na Manispaa Mkoani Ruvuma kwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Uongozi ya TASAF Abbas Kandoro, ambaye ameongoza wajumbe wa kamati hiyo kukagua miradi iliyotekelezwa na TASAF kwa kushirikiana na wananchi katika Mkoa wa Ruvuma.
  Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Uongozi ya TASAF Abbas Kandoro akisisitiza jambo kwa viongozi (hawapo pichani) wa halmashauri ya wilaya ya Songea na Manispaa ya Songea baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa miradi ya TASAF katika awamu ya pili.
  Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Uongozi ya TASAF Abbas Kandoro akielekea kukagua mradi wa maabara katika shule ya sekondari ya Mfaranyaki katika Manispaa Songea. Katika shule hii imetekelezwa miradi mitatu ambayo ni Ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa, maabara mbili na jengo la utawala vilivyogharimu shilingi milioni 197
  Kamati ya Taifa ya Uongozi ya TASAF ikikagua maabara ya kemia katika shule ya sekondari ya Mfaranyaki Mjini Songea ambako imepokea maelezo kuwa kwa hivi sasa ufaulu wa wanafunzi wanaosomea sayansi ni mzuri kuliko wanafunzi wanaosomea masomo ya sanaa baada ya kuanza kutumika kwa maabara hizo
Baadhi ya wa wajumbe wa kamati ya Taifa ya Uongozi ya TASAF wakiwa katika kikao na kamati ya ujenzi ya shule ya sekondari Mfaranyaki. Kutoka Kushoto Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu anayeshughulikia TAMISEMI Bw Zuberi Samataba, Makamu Mwenyekiti wa Kamati Tendaji TASAF Abbas Kandoro na Nyanchege Nanaghi
 Wajumbe wa kamati ya Taifa ya Uongozi ya TASAF wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukagua miradi ya TASAF katika shule ya sekondari ya Mfaranyaki Mjini SONGEA.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...