Msichana wa mjini asiyeishiwa na matukio Bongo, Lulu Mathias Semagongo ‘Aunty Lulu’, kwa mara nyingine amefanya kituko cha aina yake baada ya kuzua timbwili kisha kusaula nguo zote hadharani bila kujali yupo ukweni.
Aunty Lulu ana uhusiano wa kimapenzi na kijana anayejulikana kwa jina moja la Amani.
Habari
zisizokuwa na chembe ya ‘dauti’ zilidai kuwa hivi karibuni, Aunty Lulu
na Amani walikuwa wakipata kinywaji kwenye baa moja iliyopo jirani na
nyumbani kwa wakwe zake maeneo ya Majohe, Dar ndipo ukaibuka ugomvi kati
yao na kusababisha pachimbike.
Chanzo
hicho kutoka ndani ya familia ya wakwe zake Aunty Lulu, kilidai kwamba
mwanadada huyo alizua timbwili alipokuwa akipigana na Amani.
Ilisemekana
kwamba katika hali ya kushangaza, Aunty Lulu alikwenda mbali zaidi
alipovua nguo hadharani na kubaki mtupu hivyo kuwalazimu watu wenye
busara kumshika na kumsihi avae nguo kisha walimpeleka nyumbani
wanakoishi maeneo hayohayo ya jirani na wakwe zake.
“Yaani
Aunty Lulu anamng’ang’ania kwa nguvu ndugu yetu Amani wakati familia
nzima haimtaki kwa sababu ya tabia zake hizo, hii ni mara ya pili kuvua
nguo hadharani.
“Ukweli hata baba mkwe hataki kumsikia, ameshampigia sana kelele mwanaye aachane naye,” kilisema chanzo hicho.
Baada
ya kunyetishiwa ishu hiyo, Ijumaa Wikienda liliwasaka wahusika kwa
kuanzia na Aunty Lulu ambapo alikiri kwamba ni kweli ugomvi ulitokea
lakini hakuvua nguo.
“Ni
kweli tuligombana hapo baa lakini sikuvua nguo na kuhusu kila siku
kupigana, jamani hayo ndiyo mapenzi. Wanaosema mimi ndiye namng’ang’ania
Amani siyo kweli kwani wote tunapendana,” alisema Aunty Lulu.
Kwa upande wake Amani alifunguka: “Habari hizo siyo za kweli kabisa ndugu mwandishi.”
>>Ijumaa Wikienda
>>Ijumaa Wikienda