Unaikumbuka
nyimbo ya Ice Cream iliyoimbwa na Noorah? Ni nyimbo nzuri iliyotamba
miaka iliyopita na kuvuma zaidi baada ya video yake kutoka ambapo ndani
yake kulikuwa na Video queen aliyefahamika kwa jina la Doreen.
Taarifa
zilianza kusambaa kuwa mwanadada huyo kwa sasa ametumbukia katika tatizo
la matumizi ya dawa za kulevya huku akihitaji msaada mkubwa.
Kupita
ukurasa wa Instagram mwanamuziki Ray C ambaye nae aliwahi kukumbwa na
tatizo hilo akiweka picha yake pamoja na Doreen huku akidai kuwa
amempata na amekubali kuanza matibabu kuachana na dawa za kulevya.
Ray C ameandika kupitia ukurasa wake wa Instagram dakika chache zilizopita kuwa ”rayc1982 Mungu ni mwema sana!!tena sana!!
nilipotangaza
kuwa nimefungua taasis yangu ya kuelimisha jamii kuhusu athari za
madawa ya kulevya,nilipata emails nyingi kuhusu kumsaidia Doreen video
queen aliecheza kwenye video ya Noorah iitwayo ice cream!!nilijaribu
kumtafuta baada ya kuona picha yake kwenye website ya vibe magazine!!
roho
iliniuma sana nikamwomba Mungu anisaidie nimpate!!namshukuru Mungu
Asubuhi ya juzi Nikiwa ofisini nikaona email kutoka kwa dada yake Doreen
kichwa cha habari Kikiwa Msaada,nilipoisoma chozi lilinitoka nika reply
Mara moja nilimuomba anitumie namba yake tuongee,nikampigia akaniambia
doreen Hali yake si Nzuri kutokana na drugs,moyoni nikawa Nafikiria Huyu
dada angejua jinsi nilivyomtafuta mdogo wake !!!!!
ikawa
Kama bahati,tukaongea kwa kirefu sana na nikamwambia tukutane kitengo
cha madawa Mwananyamala!nilipomuona Doreen Kwa Mara ya kwanza nilifurahi
kupita maelezo,ila nikawa na wasiwasi kuhusu utayari wake wa kuanza
Tiba ya methadone isije ikawa amelazimishwa kuja akaniambia dada yangu
Nimechoka Maisha ya utumwa nisaidie!!
hicho
ndo nilichotaka kusikia nikamwambia Kwa uwezo wa Mungu Shetani
ameshindwa!!!!!!am soooo happy Doren ameanza Tiba ya methadone!!!wapenzi
wote wa bongo flava nawaomba tumwombee mdogo wetu aweze kusimama kwenye
Tiba na ashinde majaribu ya Shetani na aishi kwa amani bila utumwa wa
shetani.God We Trust!!!I love You my lil sister…..
Nawahamasisha
wengine huko Mliko mwenye ndugu,Jamaa au rafiki,njoo Katika taasis yetu
uweze kusaidiwa!usikubali Maisha ya utumwa wa madawa ya kulevya,njoo
tukusaidie…Ray C Foundation pamoja na Kitengo cha Methadone We love you
guys,We can help you….”
***mwisho wa kunukuu***
kuicheck video hiyo na picha zake jinsi alivyokuwa amechakaa basi usiondoke click