Mwanafunzi
wa darasa la sita shule ya msingi Ikungi mchanganyiko wilaya ya Ikungi
mkoa wa Singida, Julius Charles (12) ambaye anatumia mguu wa kulia
kuandika kutokana na kutokuwa na mikono.Pia anatumia mguu huo kutandika
kitanda chake.
MWANAFUNZI
wa darasa la sita shule ya msingi Ikungi mchanganyiko wilaya ya Ikungi
mkoani Singida,Julius Charles (12) ambaye hana mikono ameiomba serikali
imsaidie kupata mtu atakaye mhudumia ili aweze kusoma kwa uhuru zaidi
aweze kufikia lengo lake la kusoma hadi chuo kikuu.
Julius amesema amefikia uamuzi huo wa kuomba kupatiwa mtu wa kumhudumia kutokana na kutokuwa na mikono.
Amedai ulemavu huo, umesababisha pamoja na mambo mengine atumie mguu wake wa kulia kuandika na kutandika kitanda.
Julius
amefafanua zaidi kwa kusema ulemavu wake huo vile vile, unasababisha
ashindwe kuoga,kufua nguo zake na kwamba anapata taabu kubwa wakati wa
kujisaidia chooni.
Mwalimu
mkuu wa shule ya msingi Ikungi wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida, Olivary
Kamilly, akimsaidia mwanafunzi Julius Charels Kumvalisha soksi baada ya
kutoka darasani.
"Kutoa
madaftari na kalamu ndani ya mfuko,natumia mdomo wangu.Pia kwa vile sina
mikono natumia mdomo kuchukua chakula kutoka kwenye sahani",amesema.
Julius anasema binafsi anamshukuru na kumpongeza rais Kikwete,kwa moyo wake wa kuwajali walemavu wa aina mbalimbali.
"Nina
imani kwamba kama ningeonana na Rais Kikwete kwa jinsi anavyowajali
walemavu mimi mwenye uchu mkubwa wa kujisomea ataweza kunisaidia kupata
mtu wa kunihudumia.Hata hivyo,sikati tamaa kusaidiwa na Rais wetu
Kikwete.Akisoma habari hii kwenye Mtandao huu,nina hakika atanisaidia
ili ndoto yangu ya kufika chuo kikuu siku moja iweze kuwa kweli",amesema
Julius.
Kwa mujibu wa mwalimu wake,Ana Mjema, Julius kwenye mitihani mbalimbali huwa anashika nafasi ya tatu au ya nne.
Amesema
mwanafunzi huyo asiye na mikono,kwa kutumia mguu wake ana mwandiko mzuri
kuliko wanafunzi wasio na ulemavu.Pia ana kasi katika kuandika.
Mwanafunzi
wa darasa la sita shule ya msingi Ikungi mchanganyiko wailaya ya
Ikungi, Julius Charles, akitandika kitanda chake kwa kutumia mguu wake
wa kulia ambao pia anautumia katika kuandika.
Matroni
wa mabweni ya kulala wanafunzi walemavu wa shule ya msingi Ikungi
mchanganyiko wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida, Modesta Macha, akiwa na
wanafunzi wa darasa la sita Julius Charels.
Mwanafunzi
wa darasa la sita shule ya msingi Ikungi mchanganyiko wilaya ya Ikungi
mkoa wa Singida,Julius Charles,akichukua daftari lake kwa ajili ya
kulihifadhi kwenye mfuko wake. Julius anatumia mdomo kwa vile hana
mikono.(Picha zote na Nathaniel Limu).