Na. Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi.
Watu wawili wamepoteza maisha kutokana na ajali mbili zilizotokea katika maeneo mawili tofauti na nyakati
tofauti Mkoani Dodoma.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID
MISIME – SACP ameeleza kuwa, ajali ya kwanza ilitokea tarehe 30/05/2014 majira
ya saa 18:30hrs katika kijiji cha Ipala Wilaya ya Dodoma ambapo gari lenye
namba za usajili DFP 614 Toyota Land Cruiser mali ya chuo cha Serikali za Mitaa
Hombolo likitokea chuoni kuelekea Dodoma mjini likiendeshwa na ALFRED S/O
MLIGO, MIAKA 35, MHEHE, liliacha njia na kupinduka na kusababisha kifo
chake. Pia watu watano walipata maumivu
mbalimbali na walitibiwa na kuruhusiwa.
Mwili wa marehemu upo katika Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma
kusubiri taratibu nyingine.
Kamanda MISIME AMESEMA ajali ya pili imetokea majira ya saa 18:45hrs huko
katika kijiji cha SILWA barabara ya Dodoma – Morogoro ambapo gari lenye namba za
usajili T.150 CWA Toyota Granvia Station Wagon likiendeshwa na MGENI S/O
SHEMAKAME, MBONDEI, MIAKA 29 MKAZI WA MBURAHATI DSM liliacha njia na
kusababisha kifo cha GEORGE S/O TYSON, MIAKA 39, MWONGOZAJI WA FILAMU, Mkazi wa mbezi DSM.
Pia katika ajali hiyo wanahabari wanne (4) wa Mboni show walipata
majeraha mbalimbali na kutibiwa na kuruhusiwa, ambao ni:-
1. NIXON S/O KABUMBILE, MHAYA, MIAKA 31
2. GRACE D/O MEENA, MCHAGA, MIAKA 28
3. NTWA S/O KABOLE, MNYAKYUSA, MIAKA 33
4. JUSTINE S/O BAYO, MIAKA 27, MMASAI
Uchunguzi wa awali unaonyesha
ajali zote mbili zimesababishwa na mwendokasi.
Kamanda MISIME ametoa wito kwa
madereva kuepuka mwendokasi na kuwa na udereva wa kujihami ambao unasaidia dereva
kusimama bila kusababisha madhara linapotokea jambo lolote na hata kama ajali
ikitokea madhara hayawezi kuwa makubwa kama yanavyokuwa anapokuwa kwenye mwendo
wa kasi.