Nimeimaliza timu yangu!: Steven Gerrard na Phil Jagielka wakishangaa kilichowakuta mjini Sao Paulo.
`MNYAMA`
Luis Suarez akitokea katika majeruhi ya goti na kupangwa maalum kwa
kuwaangamiza England ameweza kufunga mabao mawili Uruguay ikishinda
mabao 2-1 dhidi ya Simba watatu usiku huu.
Suarez
alifunga mabao yake katika dakika ya 39, lakini mshambuliaji wa
England, Wayne Rooney akasawazisha bao hilo katika dakika ya 75 likiwa
ni bao lake la kwanza katika fainali zote za kombe la dunia alizocheza.
Wakati
England wakiamini watafunga bao la pili na kushinda mechi, alikuwa ni
Suarez tena katika dakika ya 84 alipoachia shuti kali na kumuacha Joe
Hart akiwa hana la kufanya na mpira kuzama nyavuni.
Kwa matokeo haya, England wamejiweka katika mazingira magumu kwasababu ni mechi ya pili wanapoteza.
England
inaweza kuwa timu ya kwanza katika fainali za kombe la dunia kupoteza
mechi mbili za ufunguzi na kusonga mbele kama watafuzu hapa kwa kushinda
magoli mengi na Costa Rica katika mchezo wa mwisho.
Lakini
hii inaonekana kuwa ndoto kwasabu hakuna uhakika wa England kuifunga
Costa Rica kwa beki yao mbovu ambayo huwezi kuiamini hata dakika tano.
Luis Suarez alifunga bao la pili kutokana na makosa ya beki ya England.
Mpira
mrefu uliopigwa na mlinda mlango wa Uruguay Fernando Muslera, ulimpita
kichwani nahodha Steven Gerrard, huku Gary Cahill akiwa amejisahau
kabisa, na Suarez hakucheza na `nyani`, alifumua shuti na kuwaharibia
usiku waingereza.
Wachezaji England wakiwa na huzuni baada ya kujua sasa michuano ya kombe la dunia inaweza kuwa bai bai.
Lazima abebwe: Suarez akibebwa na wenzake baada ya kufunga mabao mawili
Luis Suarez akishangilia baada ya kufunga bao la pili na la ushindi
Suarez akifunga goli
Suarez (katikati) akiachia shuti kali na kufunga bao la pili
Hatimaye
amefunga: Rooney akishangilia goli lake la kwanza katika fainali za
kombe la dunia tangua aanze kushiriki na la kusawazisha kwa England
usiku huu.
Rooney (kulia) akimalizia krosi huku kipa wa Uruguay Fernando Muslera akijaribu kumzuia.
Hapa chini ni vikosi vya timu zote mbili na viwango vyao. Alama ni juu ya 10.
Kikosi
cha Uruguay: Muslera 6, Gimenez 6, Godin 6, Caceres 6, Pereira 6;
Lodeiro 7 (Stuani 67, 6), Gonzalez 6 (Fucile 78), Arevalo Rios 6,
Rodriguez 6; Cavani 7, Suarez 8 (Coates 89). Subs: Munoz, Gargano,
Hernandez, Forlan, Perez, Ramirez, Maxi Pereira, Silva.
Kadi ya njano: Godin.
Mfungaji: Suarez 39, 84.
Kikosi cha England: Hart 6, Johnson 5.5, Cahill 6, Jagielka 5, Baines 5.5; Gerrard 5.5, Henderson (Lambert 87) 6; Sterling 5 (Barkley 64, 6), Rooney 6, Welbeck 4.5 (Lallana 71, 6), Sturridge 6.5. Subs: Foster, Wilshere, Lampard, Smalling, Jones, Milner, Shaw, Forster.
Kocha: Roy Hodgson 6.5
Kadi ya njano: Johnson.
Mfungaji: Rooney 75.
Mchezaji bora wa mechi: Luis Suarez.
Mwamuzi: Carlos Velasco Carballo (Spain).
Viwango na MARTIN KEOWN
Kadi ya njano: Godin.
Mfungaji: Suarez 39, 84.
Kikosi cha England: Hart 6, Johnson 5.5, Cahill 6, Jagielka 5, Baines 5.5; Gerrard 5.5, Henderson (Lambert 87) 6; Sterling 5 (Barkley 64, 6), Rooney 6, Welbeck 4.5 (Lallana 71, 6), Sturridge 6.5. Subs: Foster, Wilshere, Lampard, Smalling, Jones, Milner, Shaw, Forster.
Kocha: Roy Hodgson 6.5
Kadi ya njano: Johnson.
Mfungaji: Rooney 75.
Mchezaji bora wa mechi: Luis Suarez.
Mwamuzi: Carlos Velasco Carballo (Spain).
Viwango na MARTIN KEOWN