SIKILIZA KIPANDE HICHO HAPO JUU HADI MWISHO USIKIE WAKATI WATANGAZAJI HAO WAKITANGAZA KUZIPOTEZEA HABARI ZA UKAWA KUANZIA LEO
Na Karol vicent
SAA chache kupita Baada Radio ya Clauds Fm kutangaza Rasmi kutozisoma Habari zozote zinazowahusu Wajumbe wanaunda umoja wa Kutetea Katiba ya Wananchi UKAWA, kwa kile wananachodai Umoja huo hauna jipya bali unataka umaharufu tu.
Na Karol vicent
SAA chache kupita Baada Radio ya Clauds Fm kutangaza Rasmi kutozisoma Habari zozote zinazowahusu Wajumbe wanaunda umoja wa Kutetea Katiba ya Wananchi UKAWA, kwa kile wananachodai Umoja huo hauna jipya bali unataka umaharufu tu.
Kauli hiyo ya ambayo inakwenda kinyume na Maadili ya Vyombo vya
Habari imetolewa leo na Mtangazaji wa Kipindi cha Power breakfast Babra
hassani wakati wakichambua magazeti ya siku ambapo alisema kwa
sasa hawatazisoma habari zozote zinazohusu umoja huo wa Ukawa kwa madai
umoja huo ni wabinafsi na hawana jipya bali wanataka Umaharufu.
Naye Mwanasheria wa Umoja wa kutetea katiba ya Wananchi
UKAWA ,Tundu Lissu amewavaa na kusema Radio hiyo inajimaliza na ndio
itakuwa inaonekana wazi inapendelea Upande moja Kisiasa.
Kauli hiyo Tundu Lissu,ameitoa mda huu wakati alipokuwa anaongea
na Mwandishi wa Mtandao huu,Kuhusu wao Ukawa wamepokeaje Taarifa hiyo
ya kutosomwa Habari zao kwenye Radio hiyo.Ambapo Lissu alisema hizo
taarifa anazisikia na kama ni kweli wametangaza hivyo watakuwa
wamejimaliza.
“Kwanza nimezisikia hizo taarifa na kama kweli aliyosema huyo
mtangazaji ndio msimamo wa Radio nzima basi watakuwa watu wa Ajabu sana
maana leo Nchi nzima habari ya Mjini ni Ukawa,leo utasemaje ukawa ni
wabinafsi wakati wasomi na watu wengine wanaungana na sisi leo inakuwaje
Radio hiyo iseme hivyo kama wako upande mmoja wa Kisiasa weseme”alisema
Lissu.
Tundu Lissu,ambaye naye ni Mjumbe wa Bunge maalum la Katiba
alizidi kusema yeye sio mwanahabari bali anachokijua huo utakuwa msimamo
wa Radio nzima na wao Ukawa hawata ogopa na kuacha kuwatetea wananchi
kwani wako kwa ajili ya kuwakomboa wananchi na hawezi kukatishwa na
tamaa na watu wachache wenye maslai ya upande mmoja.
“Harafu inashangaza sana leo nchi nzima inazungumzia Ukawa harafu
mtua aseme leo Ukawa utotangaza habari zao kwa misingi hipi?”alihoji
Tundu lissu.
Kauli hiyo ya Tundu Lissu,imetolewa saa chache kupita baada
Mtangazaji wa kipindi cha Power Breakfast Babla Hassani,kutangaza Rasmi
kwamba hawatasoma Habari zozote zinazohusu Umoja huo.
“Mimi Naona kusoma Story zinahusu Ukawa tunawapa kiki tu wao
siwamekuwa kutupotezea kutorejea Bunge I whon doing,vile vikao
vinawanufaisha watanzania wote wao ni wabinafsi tu,the best ican do
tuwapotezea Habari zao, na ukiona habari inahusu Ukawa tu usisome hapa
kwenye Redio,na wakae huko nje atuwataki Ukawa bungeni”alisema Babla
Hassani.
Kauli hiyo ya iliungwa Mkono pia na Mtangazaji wa mwengine wa
kipindi hicho, Paul Jems anayejulikana kwa jina la Umaharufu “PJ” naye
alisema kwanzia sasa hatazisoma habari zozote zinazohusu Umoja huo kwani
wanapoteza pesa za wananchi bure kwa kususia bunge hilo.
Msimamo huo wa Watangazaji hao unakwenda Kinyume na Mmiliki wa
Radio hiyo ya Clauds Fm Joseph Kusaga alipokuwa anahojiwa na kipindi
kimoja cha runinga kutoka nchini Uingereza kinachojulikana,The Sporah
Show ambapo katika kipindi hiko alisema Radio yake haina upande wowote
wa Kisiasa na kuongeza ni Redio huru inayofanya kazi bila kushabikia
upande wowote.
Lakini kwa sasa kauli ya Mmiliki hiyo inakwenda tofauti na
ilivyo,na kama Radio ikifanya kama inavyofanya hivyo kwa sasa,Basi Redio
hiyo itapelekea machafuko makubwa kama yaliyowai kutokea nchini Rwanda
na kuua maelfu ya watu,na sababu kubwa ni Radio za nchini humu zilikuwa
na misimamo kama walioyonayo Clauds.
Umoja huo wanaupinga wa Ukawa unaundwa na Muunganiko wa
Vyama vikuu vya Upinzani ikiwemo Chama cha demokrasia na Maendeleo
CHADEMA,Chama cha wananchi CUF,Chama cha Mageuzi NCCR,ND pamoja na
Baadhi ya wajumbe 201 walioteuliwa na Rais Kikwete.