MWANAMITINDO maarufu
ambaye aliwika na lebo ya Kidoti, Jokate Mwengelo juzikati aliamua
kujizamisha rasmi kwenye muziki wa Bongo Fleva baada ya kupanda kwa mara
ya kwanza katika Jukwaa la Serengeti Fiesta 2014, akiwa na madensa
wake.
Ishu hiyo ilitokea usiku wa kuamkia Agosti 10 mwaka huu ndani ya uwanja
wa CCM Kirumba jijini Mwanza, ambapo Jokate ‘aliwa-suprise’ mashabiki
akiwa anajiamini akiimba na kutawala steji.Kwa muda wote akiwa jukwaani,
mwanamitindo huyo alicheza staili sambamba na wanenguaji wake pasipo
kupotea hata mara moja kama vile alianza zamani kuimba.
“Nina kipaji cha kuimba, na ndiyo maana nimekuwa nikiimba kanisani siku
zote, muziki naupenda sema mwanzo nilishindwa kwenda na mambo mawili kwa
wakati mmoja, ila sasa ndiyo nimezindua rasmi harakati za muziki na
siku chache zijazo nitaachia video ya wimbo wangu nilioimba leo,”
alisema Jokate.