LADY JAY DEE "KOMANDO" KUINGIA BONGO TAREHE 3 BAADA YA KUCHUKUA TUZO YA AFRIMMA!

Lady Jay Dee ambaye ameshinda tuzo ya AFRIMMA kama mwimbaji bora wa kike Afrika Mashariki atatua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, August 31 mwaka huu akitokea Marekani.
Akiongea na tovuti ya Times Fm, meneja wa Lady Jay Dee, Captain Gardener G. Habash amesema kuwa mwimbaji huyo anatarajia kuondoka Houston, Marekani August 1 na kuingia Dar es Salaam August 3. 

Amesema Lady Jay Dee yuko Marekani alikuwa ameenda kwa ajili ya likizo au mapumziko. Tuzo hiyo ya AFRIMMA imekuwa tuzo ya 30 kwa muimbaji huyo, idadi hiyo ilifahamika rasmi baada ya kuandika ujumbe wa shukurani kwa mashabiki wake.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...