Home »
Uncategories »
NGONO MWANZO MWISHO!!!!!!!! KIJIJI CHA UFUSKA (KUUZA URODA) CHA FUMULIWA MBAGALA
NGONO MWANZO MWISHO!!!!!!!! KIJIJI CHA UFUSKA (KUUZA URODA) CHA FUMULIWA MBAGALA
Unknown
2:23 PM
SIKU
chache baada ya gazeti la Ijumaa kuibua danguro la vigogo maeneo ya
Kinondoni jijini Dar es Salaam na wahusika kutiwa mbaroni na polisi,
mwishoni mwa wiki waandishi wamekifumua kijiji cha ufuska.Kijiji
hicho kilichogunduliwa Mbagala Zakhem, jijini Dar, wasichana na
wavulana walinaswa wakifanya vitendo vya ngono kwenye moja ya mabanda
ambayo yametengenezwa maalumu kwa shughuli hiyo.Awali,
waandishi wetu walipata taarifa kutoka kwa wasamaria za kuwepo kijiji
hicho pembezoni mwa barabara ya kwenda Kiburugwa, hivyo kuamua
kufuatilia.
Operesheni
hiyo ilifanywa na waandishi kwa kushirikiana na jeshi la polisi
Jumamosi iliyopita usiku ambapo ilifanikiwa kuwanasa baadhi ya vijana
akiwemo mwanamke mmoja aliyekutwa akifanya ngono na wanaume wawili
(walio pichani).Hata
hivyo, kundi la watu kama wanane wakiwa na nguo mikononi walitimua mbio
baada ya kuona polisi wamevamia chumba kimoja kilichotengenezwa kwa
uzio wa vipande vya magunia chakavu na makaratasi walichokuwa
wakikitumia kufanyia ngono.
Aidha,
wana usalama walifanikiwa kuwakamata watu watatu, wanaume wawili pamoja
na mwanamke aliyejitambulisha kwa jina moja la Semeni waliyekuwa
wakifanya naye mapenzi.Baada ya kuwatia mbaroni watu hao na kuwafanyia upekuzi, walikutwa na kondomo na vipisi vya bangi.
Maafande
walipomhoji Semeni alisema vijana hao walimlipa shilingi 5,000 kila
mmoja na mmiliki wa eneo hilo aliyemtaja kwa jina moja la Babu walimlipa
shilingi 2,000.Mtu mmoja aliyeshuhudia tukio hilo, aliwapongeza polisi kwa kufanikiwa kuwakamata baadhi ya vijana hao.
“Kwa
kweli sehemu hii ni kama kijiji cha ngono maana hata wanafunzi
huchukuliwa na kuingizwa kwenye vibanda hivi kwa ajili ya kufanya
ufuska, tunashukuru kwa kuamua kukisambatisha,” alisema jamaa huyo
aliyeomba hifadhi ya jina lake.
![](https://lh3.googleusercontent.com/blogger_img_proxy/AEn0k_s-ClacqP1EHRyWI0g8ezq7LTx0u6-gPohdvUN42uYGsc8bFFCuG00y3F9vT1pP8_b21T-yXT7TKUZh8frN3mcw8fwRHeqpc9Jmw86xGhJ8VDL058I-Nxtp5UbsMvdrBesFHXLFma_GMXdozddHque4ObRgTVDFyOdvvAJ4YmTkVFzSK2J4yDT724gRqL9un2vbs_w55hNY2WZt2FSf8odLzrm2jYHzIH2dGZAF6Z3_OMjfFuAxVOXL2ZOmlpE=s0-d)