Bao hilo lililoipa ushindi Ujerumani limefungwa na Mario Gotze dakika ya 113 ya mchezo na kuifanya timu hiyo kutwaa Kombe la Dunia mara ya nne baada ya mwaka 1954, 1974 na 1990.
Katika michuano hiyo, kipa wa Ujerumani, Manuel Neuer ametwaa tuzo ya kipa bora, Lionel Messi wa Argentina akitwaa tuzo ya mchezaji bora huku mshambuliaji wa Colombia, James Rodriguez akiwa ndiye mfungaji bora baada ya kutia kambani mabao sita.