UJERUMANI VS ARGENTINA: MTOTO HATUMWI SOKONI LEO

NI Ujerumani vs Argentina usiku wa leo.
MIAMBA miwili ya soka duniani, Ujerumani na Argentina inakutana kwa mara nyingine katika fainali za Kombe la Dunia 2014 usiku huu katika Uwanja wa Maracana, Rio de Jeneiro nchini Brazil.
Staa wa Argentina, Lionel Messi.
Timu hizo zinakutana kwa mara ya tatu katika fainali za Kombe la Dunia ambapo mwaka 1986 zilikutana katika fainali iliyopigwa nchini Mexico na Argentina kutwaa kombe baada ya ushindi wa mabao 3-2.
1990 timu hizo zikakutana tena katika fainali iliyochezwa Italia ambapo Ujerumani waliibuka kidedea kwa bao 1-0 na kutwaa kombe. Leo wanakutana Brazil, kitendawili kinabaki, ni nani atamfunga mwenzake na kutwaa kombe?
Nyota wa Ujerumani aliyeweka rekodi ya upachikaji mabao katika Kombe la Dunia akiwa jumla ya mabao 16, Miroslav Josef Klose.
Ujerumani wametwaa kombe hilo mara tatu mwaka 1954, 1974 na 1990 huku Argentina wakilitwaa mara mbili mwaka 1978 na 1986.
Iwapo Ujerumani watashinda watakuwa wamelitwaa kombe hilo mara nne sawa na Italia na iwapo watashinda Argentina watakuwa wamelitwaa mara tatu sawa na Ujerumani.
Orodha ya washindi wa kombe hilo tangu mwaka 1930 ni kama ifuatavyo:
MWAKA
MSHINDI
1930
Uruguay
1934
Italia
1938
Italia
1950
Uruguay
1954
Ujerumani Magharibi
1958
Brazil
1962
Brazil
1966
England
1970
Brazil
1974
Ujerumani Magharibi
1978
Argentina
1982
Italia
1986
Argentina
1990
Ujerumani Magharibi
1994
Brazil
1998
Ufaransa
2002
Brazil
2006
Italia
2010
Hispania
2014
 ?
Mpaka sasa, Brazil ndiyo wanaongoza kutwaa kombe hilo kwa mara tano wakifuatiwa na Italia iliyolitwaa mara nne, Ujerumani mara tatu, huku Uruguay na Argentina wakilitwaa mara mbili kila mmoja. Hispania, England na Ufaransa kila mmoja amelichukua mara moja.
ZAWADI
Bingwa wa mwaka huu ataondoka na kitita cha dola milioni 35 sawa na shilingi bilioni 58.2, mshindi wa pili akilamba dola milioni 25 sawa na shilingi bilioni 41.6 huku mshindi wa tatu akikomba dola milioni 22 sawa na shilingi bilioni 36.6 na mshindi wa nne akiweka kibindoni dala milioni 20 sawa na shilingi bilioni 33.3.
Timu nne zitakazoaga mashindano hayo katika hatua ya robo fainali zitachukua dalo milioni 14 kila mmoja sawa na shilingi  bilioni 23.3.
Timu nane zilizoondolewa katika hatua ya 16 Bora zitachukua dola milioni 9 kila mmoja sawa na shilingi bilioni 15 na timu 16 zilizoondolewa katika makundi kila mmoja atachukua dola milioni 8 sawa na shilingi bilioni 13.3.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...