SHAKIRA, WYCLEF JEAN KUIPAMBA FAINALI YA KOMBE LA DUNIA LEO USIKU

Shakira atapanda sejini kuimba wimbo wa "La la la (Brazil 2014)".
WANAMUZIKI Shakira na Wyclef Jean, usiku wa leo wataongoza burudani katika fainali za Kombe la Dunia 2014 kati ya Ujerumani na Argentina.
Staa wa Hip Hop kutoka Haiti, Wyclef Jean naye atakuwepo kutoa kburudani usiku huu.
Mastaa wengine watakaoangusha burudani usiku wa leo ni pamoja na mpiga gitaa mahiri wa Mexico, Carlos Santana, Ivete Sangalo, Alexandre Pires wa Brazil na wanamuziki kutoka Shule ya Samba nchini Brazil.
Burudani hizo zitaanza saa 2:30 usiku ikiwa ni saa moja na nusu kabla ya mtanange wa fainali kuanza katika Uwanja wa Maracana, Rio de Janeiro, Brazil.
Mpiga gitaa mahiri wa Mexico, Carlos Santana naye ndani.
Shakira ambaye anafanya shoo yake ya tatu katika Kombe la Dunia, atapanda stejini kuimba wimbo wake wa "La la la (Brazil 2014)" huku staa wa Hip Hop kutoka Haiti, Wyclef Jean na Alexandre Pires wakiimba wimbo "Dar um Jeito (We Will Find A Way)" wakati mashabiki wakiingia uwanjani.
Katika fainali za 2010, Afrika Kusini, Shakira aliimba wimbo wa "Waka Waka" huku 2006 nchini Ujerumani akiimba "Hips Don't Lie".
Shakira.
Kombe litakabidhiwa kwa mabingwa na Rais wa Brazil, Dilma Rousseff na Rais wa FIFA, Sepp Blatter.
Kabla ya mechi, aliyekuwa beki wa Barcelona, Carles Puyol na modo wa Brazil, Gisele Bundchen wataliingiza kombe hilo uwanjani.
Ulinzi umeimarishwa katika fainali ya leo ambapo askari 26,000 watakuwa mitaani kudumisha ulinzi.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...