
Zifuatazo
 ni kauli zilizotolewa na viongozi mbalimbali wa zile kamati kwenye 
bunge la katiba linaloendelea sasa hivi hapa Dodoma ambapo viongozi hawa
 leo April 14 2014 wameendelea kuwasilisha taarifa kutoka kwenye kamati 
zao,
Ni
 maoni ya pande mbili ambazo ni maoni ya wengi ambao ndio wanaounga 
mkono serikali mbili alafu maoni ya wachache ambao wanaunga mkono uwepo 
wa serikali tatu.
Tundu Lissu: ‘Nusu
 karne ya uongo iishe, Tanganyika iliuwawa na amri za Mwalimu Nyerere na
 hakuwa na mamlaka kisheria kuiua, hatujawahi kuwa nchi moja, habari ya 
Tanzania kuwa nchi moja iliingizwa ktk katiba miaka 20 baada ya 
muungano, nchi hii ni haramu…. miaka 50 ya kudanganyana ikome, nchi hii 
inahitaji kuelezwa ukweli’
Mchungaji Mtikila:
 ‘tulijengwa kwenye misingi ya uongo ndio maana Mungu alishindwa 
kubariki hii nchi yetu kwa miaka 50, uongo tuuondoe, swala la muungano 
lilikua utapeli wa kisiasa, tuurudie ukweli kuhusu uhuru wa Watanganyika
 na Wazanzibari’
Mh Wassira: ‘Hati
 ya Muungano ipo, naahidi kwa niaba ya Jamuhuri itawasilishwa kwa 
Mwenyekiti ndani ya siku mbili zijazo, kama Wananchi wangetoa maoni 
kutaka kuvunja muungano, je tume ingeyaleta? serikali 3 italeta 
mgongano’
Mh Wassira: ‘Katiba
 ya Znz ndio itabakia kuwa sheria kuu kwa Znz kwa mambo yasiyokua ya 
muungano, tukiweka serikali 3 hapa zikaweka masharti kuna watu watapata 
matatizo, itapunguzia Wazanzibari fursa’
Ismail Jussa: ‘Hoja
 za historia kwamba tulikua vipi haziwezi kulibakisha taifa katika 
mgando, ukiangalia katiba ya muda ya mwaka 1965 inaendelea kuitambua 
Tanganyika na kuwepo makamu wawili wa Rais’
Ismail Jussa: ‘Mkataba
 wa muungano haukutoa mamlaka kwa chombo chochote kubadilisha kilichopo 
ndani, ajabu bunge limefanya, tunapokua Znz tunasema mengine tukija huku
 tunaufyata, Wazanzibari watatuhukumu’
Ismail Jussa:
 ‘Zanzibar tumeachwa watupu, tumechoka na hatukubali tena, ktk mfumo wa 
serikali mbili Zanzibar haitaweza kujisimamia kamwe, hatutakubali 
kuendelea nao’
Ismail Jussa: ‘Kama kuna nia njema kwa nini kuna kufichaficha, mfano mwingine hai ni Rais wa Znz kuondolewa kuwa makamu wa Rais’
CHANZO: MILLARDAYO.COM
