Waziri
Prof. Mark Mwandosya ametoa taarifa bungeni mjini Dodoma kuhusu ajali
ya helkopta iliyomkumba makamu wa rais Dkt. Mohamed Gharib Bilal na
ujumbe wake jana na kusema wamepata majeraha madogo madogo lakini si ya
kutisha.
Prof.
Mwandosya amesema ni jambo la kumshukuru Mungu kuwa wote waliokuwa
kwenye helkopta hiyo wamenusurika kifo na wapo salama salimini.
Amesema
maeneo mengi ya nchi yamekumbwa na maafa ikiwemo Dar es salaam, Pwani,
Morogoro na mikoa mingine yamekumbwa na mafurikio ikiwemo kuharibika kwa
miundombinu hasa ya barabara na serikali imeshaanza jitihada za
kuhakikisha miundombinu hiyo inatengenezwa mara moja na kurudi katika
hali yake ya kawaida.
Pia
waziri Mwandosya amependekeza posho ya leo ya wabunge wa bunge maalum
la katiba kujitolea posho ya leo ili iwe maalum kwa waathirika wa
mafuriko sehem mbalimbali za nchi.
Baada
ya kuwasilisha taarifa hiyo Mwenyekiti wa bunge maalum la katiba Mh.
Samwel Sitta amesema suala hilo litaenda kujadiliwa kwenye kamati maalum
ambayo ina kikao chake leo na itatoa taarifa kwa bunge mara baada ya
kujadili