Staa wa wimbo wa Nakomaa na Jiji, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ akiwa na mpenzi wake Nuhu Mziwanda.
Shilole alisema mpenzi wake huyo
aligundua kwamba aliteswa na wivu na kusababisha wagombane hivyo
alipotambua kosa lake, aliomba msamaha wakarudiana na mambo yakawa
swari.
Zuwena Mohamed ‘Shilole’
“Kikubwa ni kwamba ameomba msamaha
ndiyo maana na mimi sikuwa na hiyana, nikapatana naye siku chache tu
baada ya kugombana,” alisema Shilole.Hivi karibuni wawili hao
waliripotiwa kuwa wamegombana na kila mtu kuchukua hamsini zake.