KATIBU WA CCM MKOA WA IRINGA AFARIKI DUNIA

Waombolezaji ndugu na jamaa wakitoa jeneza na aliyekuwa katibu wa CCM mkoa wa Iringa Hospital ya rufaa ya mkoa wa Iringa  leo.
Mwili wa marehemu ukiwasili nyumbani kwake Gangilonga Iringa  leo kwa heshima za mwisho.
Mwenyekiti  wa CCM mkoa  wa  Iringa Jesca msambatavangu (kulia) akilia kwa uchungu kushoto ni mwenyekiti wa CCM Iringa mjini Abed Kiponza.
Askari akiweka sahihi katika kitabu cha maombolezo leo.
Mkuu wa mkoa  wa Iringa Dr Christina Ishengoma (kulia) akimpa  pole mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu kwa  kifo cha aliyekuwa katibu wa CCM mkoa Bw Emanuel Mteming'ombe.
Meneja  wa Tanroad mkoa wa Iringa Paul Lyakurwa akisaini kitabu cha maombolezo leo.
CHAMA cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa  kimepata pigo kubwa baada ya aliyekuwa   katibu  wa CCM mkoa   Emmanuel Mteming'ombe kufariki dunia usiku  wa kuamkia leo akiwa katika Hospital ya Rufaa ya   mkoa  wa Iringa.
Akizungumza na Francis Godwin juu ya kifo hicho katibu msaidizi mkoa  wa Iringa Jimson Mhagama  alisema  kuwa Mteming'ombe alikuwa akisumbuliwa na tatizo la ugonjwa  wa figo na Pumu.

Alisema kuwa Mteming'ombe  alikuwa amelazwa katika  Hospital ya  Rufaa ya  mkoa  wa Iringa kwa zaidi  ya siku  tatu  sasa akitibiwa.

Hata  hivyo  alisema  kuwa maradhi  hayo yalimfanya  kushindwa  kufika ofisini  toka Novemba 27 mwaka huu siku ambayo mkoa  wa Iringa  ulipata  kuhitimisha mbio  za bendera.

Mwenyekiti wa CCM mkoa  wa Iringa Jesca Msambatavangu alisema  kuwa  kifo  cha katibu  huyo  kimeacha  pigo  kubwa kwa  chama hasa  ukizingatia  kuwa mchango  wake  ulikuwa  ukihitajika  sana katika uhai  wa CCM mkoa wa Iringa.

Msambatavangu  alisema  kuwa mazishi  ya katibu  huyo yanataraji kufanyika kesho  Desemba 20  katika  kijiji  kwake Mageha mjini Rujewa wilaya ya Mbarali mkoa  wa Mbeya.

Alisema  kuwa miongoni  mwa viongozi  wa CCM Taifa  wanaotarajia  kushiriki mazishi  hayo ni  pamoja na naibu katibu mkuu wa CCM Mwingulu Nchemba na  viongozi  mbali mbali  wa  chama na serikali  kutoka ndani ya mkoa wa Iringa na nje  ya mkoa.

Msambatavangu  alisema  kuwa CCM mkoa  wa Iringa itaendelea  kumuenzi Mteming'ombe kwa  kuendeleza  yale  yote  aliyeyatenda katika  chama mkoa .

Huku  mwenyekiti  wa CCM wilaya ya Iringa mjini Abed Kiponza akizungumzia  juu ya  kifo  hicho  alisema  kuwa alipokea kwa mshituko  mkubwa taarifa ya  kifo  hicho baada ya  kupokea  simu majira ya saa 8 usiku .

Kiponza  alisema kuwa CCM mkoa na taifa  imempoteza  kiongozi mchapakazi ambaye  katika uongozi  wake  alikuwa na ushirikiano mzuri  kwa  kila mmoja bila kubagua.

Miongoni  mwa viongozi wa chama  na  serikali mkoa  wa Iringa  waliofika nyumbani kwa marehemu Gangilonga Iringa   kutoa  heshima  zao za mwisho jana ni pamoja na mkuu wa mkoa  wa Iringa Dr Christine Ishengoma, katibu  tawala wa  mkoa wa Iringa  Wamoja Ayub , meneja wa Tanroad mkoa  wa Iringa Paul Lyakurwa ,mjumbe wa NEC mkoa wa Iringa Mahamud Madenge , kamanda wa UVCCM mkoa wa Iringa  salim Asas, kamanda wa UVCCM wilaya ya Iringa  vijijini Arif Abri na  wengine wengi.

Mdogo  wa marehemu Bw  James Mteming'ombe alisema kuwa marehemu alizaliwa  mwaka 1956  na  kuwa ameacha mke  mmoja na  watoto  watatu.


CHANZO NI FRANCIS GODWIN BLOG


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...