Mchezaji wa Club ya Barcelona, Lionel AndrĂ©s Messi mwishoni mwa mwaka 2013 alitua Tanzania kimya kimya kufanya tangazo la Turkish Airlines kwenye Mlima Kilimanjaro.Idea ya tangazo hilo ni kuwa Messi na mchezaji wa mpira wa kikapu wa timu ya Los Angeles Lakers, Kobe Bryant wanashindana kupiga picha bora zaidi aina ya selfie. Tangazo linaanza kwa Messi kumtumia picha Kobe yake mwenyewe akiwa mbele ya kanisa la Saint Basil’s Cathedral mjini Moscow.
Kobe naye anajibu mapigo kwa kwenda kwenye kuta maarufu za China (The Great Wall of China) na mashindano yanaendelea hadi kumfanya Messi aje kuchukua selfie kwenye mlima Kilimanjaro, huku maeneo yote hayo yakifikika na ndege za Turkish Airlines. Mwisho Messi anajipiga picha akiwa Sultanahmet Square mjini Istanbul, na kuja kugunduaa nyuma yake alikuwepo Kobe aliyetokea pia kwenye picha yake.
Tazama tangazo lao hilo ambalo tangu liwekwe December 3 limeshaangalia kwa zaidi ya mara milioni 135.