Mhe.
Balozi Mulamula akiingia ukumbini kwenye sherehe ya kumkaribisha rasmi
nchini Marekani iliyoandaliwa na jumuiya ya Watanzania DMV siku ya
Jumamosi Novemba 9, 2013 Lanham, Maryland na kuhudhuriwa na Watanzania
kutoka majimbo mbalimbali wakiwemo viongozi wa jumuiya ya New York.
Rais
wa Jumuiya ya Watanzania DMV bwn. Idd Sandaly akiongea na Watanzania na
marafiki zao waliofika kwenye sherehe ya kumkaribisha rasmi Balozi
Mulamula siku ya jumamosi Novemba 9, 2013 iliyofanyika Lanham, Maryland,
machache aliyoongea Rais wa jumuiya ni msisitizo wa Watanzania DMV
kujiunga na jumuiya kwani umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu na
baadae alimkaribisha Mhe. Balozi Liberata Mulamula.
Mhe.
Balozi Liberata Mulamula akicheza wimbo huku akisindikizwa na wakina
mama na watoto wa darasa la kiswahili DMV wakati alipokua akielekea
kuongea na Watanzania waliofika kumsikiliza.
Juu
na chini ni Balozi Liberata Mulamula akiongea na Watanzania DMV siku ya
Jumamosi Novemba 9, 2013 Lanham, Maryland pamoja na mambo mengi
aliyoongea hotuba yake iliwasisimua wengi kiasi cha kumshangilia kwa
wimbo wa "Balozi sema, sema usiogope sema" alianza kwa kumsifia Balozi
aliyepita Mhe. Mwanaidi Maajar kwamba amevaa viatu vyake ambavyo kwake
yeye ni vikubwa na aliwaasa Watanzania kujiunga na jumuiya za Wanzania
na kusisitiza wasigawanyike kwa msingi ya tofauti zao za dini, itikadi
au rangi na kuwaomba viongozi wa jumuiya kuwa wabunifu wa mambo ya
msingi ambayo yanamanufaa kwa Mtanzania aishiye ughaibuni akatoa mfano
wa Bima ya maisha na maswala ya uhamiaji huku akisisitiza kwa kusema
tusiwe wachoyo wakupeana siri za mafanikio ya mambo yenye manufaa na
yatakayomsaidia Mtanznia mwenzako, kama wewe
Juu
na chini ni Watanzania na marafiki zao wakimsikiliza mhe. Balozi wakati
alipokua akiongea na Watanzania kwenye sherehe ya kumkaribisha rasmi
iliyoandaliwa na jumuiya ya Watanzania DMV.
Juu
na chini Balozi Liberata Mulamula akipongezwa kwa hotuba yake
nzuriiliyowagusa wengi aliyotoa kwenye sherehe ya kumkaribisha rasmi
iliyoandaliwa na jumuiya ya Watanzania DMV.