Jiji la Eldoret kaunti ya Uasin Gishu nchini Kenya leo lilishuhudia
tukio la kushangaza baada ya maiti iliyokuwa inasafirishwa kwa maziko
kukataa safari hiyo.
Kizaazaa kilizuka pale gari lililokuwa limelibeba jeneza lenye mwili
wa marehemu kupata hitilafu na licha ya kubadilishwa gari jingine, nalo
pia lilikataa kuwaka.
Hapo ndipo marafiki na jamaa ya marehemu walipochukua fursa ya kuirai maiti hiyo ili ipate kufikishwa eneo la maziko.
Baada ya maombi ya takribani saa moja kutoka kwa ndugu na jamaa wa
marehemu kuiomba maiti hiyo ikubali kusafirishwa, hatimaye safari
ilianza na kuacha maswali mengi yasiyo na majibu kwa mashuhuda wa tukio
hilo.
(CHANZO: KTN)