HII NDIYO TOP 5 YA MASTAA WASIOUZA, WANAOUZA KWENYE FILAMU

UTAFITI wa kina umefanyika, wadau wamehojiwa, wakatoa maoni kuhusiana na mastaa wa kike wa sinema za Kibongo ambao wasiofanya vizuri sokoni (wasiouza) na wale wanaouza zaidi.
Jacqueline Wolper.
Ijumaa Wikienda linayaanika majina 10 yaliyopatikana kwa kuzingatia maoni  yaliyogawanywa katika kipimo cha asilimia mia moja.
Kwenye utafiti huo, wadau 1000 waliulizwa maswali. Maswali yalikuwa mawili; msanii gani hauzi/havutii sokoni kwa sasa na nani anauza zaidi? Wakapatikana wasanii kumi, watano wasiouza na ya wengine watano wanaouza zaidi sinema zao.
Imebainika kuwa, katika listi ya wasanii watano wasiouza (Top 5), watu wengi waliwakosoa wasanii husika kwa kopoteza mvuto sokoni hivyo hata pato lao lililotokana na uzalishaji wa sinema, limepungua kama siyo kufa kabisa.
Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Ifuatayo ndiyo Top 5 ya wasanii wa kike wasiouza sinema kutokana na majibu ya utafiti:
Anayeongoza ni Irene Uwoya ambaye amepata asilimia 40 kati ya mia za kutouza. Uwoya kwa sasa ametangaza kuachana na uigizaji na kujikita katika utangazaji, imedaiwa kuwa ameamua kufanya hivyo baada ya kuona kila sinema anayoingiza sokoni inabuma, amejaribu upepo kwenye utangazaji.
Chuchu Hansi ameshika nafasi ya pili, amepata asilimia 20 za kutouza. Imeelezwa sinema zake zimekosa mvuto sokoni, kila akijitutumua kuinuka anaambulia patupu. Anafuatiwa na Rachel Haule ambaye amepata asilimia 25.
Nafasi ya nne imekwenda kwa Yobnesh Yusuf ‘Batuli ambaye amepata asilimia 15 na anayekamilisha Top 5 ni Jacqueline Pentezel aliyepata asilimia 5.
Kwa upande wa wasanii wanaouza, utafiti umebaini anayeongoza Top 5 ni Jacqueline Wolper (35%), Elizabeth Michael ‘Lulu’ (20%), Wema Sepetu (20%), Wastara Juma (15%) na wa tano ni Riyama Ally (10).
Wasanii hao wametofautiana katika asilimia kutokana na kura nyingi za kukubalika sokoni.


Source: GPL


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...