Mkurugenzi
wa Elimu ya juu, Wizara ya Elimu na mafunzo ya Ufundi, Profesa Sylvia
Temu ambaye alikuwa mgeni rasmi aliyemwakilisha Waziri wa Elimu na
mafunzo ya Ufundi akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa mpango wa
utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wanaosoma vyuo vya nje ya nchi
uliofanyika jana katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Kaimu
Katibu mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania, Profesa Magishi Nkwabi
Mgasa akiwapongeza kampuni ya Global Education Link kwa kushirikiana na
Benki ya Afrika (BOA) kwa kuweza kubuni njia itakayowawezesha wanafunzi
wengi waliokuwa wanapenda kwenye kusoma nje ya nchi ila wanakosa pesa.
Vile vile aliwaomba wanafunzi kuacha kukurupukia vyuo vya nje bila
kutambua kama vinatambulika Tanzania ama lah ili kuwaepushia
usumbufu. Uzinduzi huo ulifanyika jana katika hoteli ya Serena jijini
Dar es Salaam.
Naibu
katibu mkuu Tamisemi, Zuberi Samataba akiongea machache katika uzinduzi
wa utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wanaosoma vyuo vya nje ya nchi
uliofanyika jana katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mtendaji na mwanzilishi wa taasisi ya Global Education Link, AbdulMalki
Molel akitoa maelezo jinsi mpango wa utoaji wa mikopo kwa wanafunzi
wanaosoma vyuo vya nje ambapo jna ilikuwa ndiyo uzinduzi katika hoteli
ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya Afrika Tanzania, Ammish OWUSU-AMOAH akitoa hotuba
yake wakati wa uzinduzi wa mpango wa utoaji wa mikopo kwa wanafunzi
wanaosoma vyuo vya nje ya nchi uliofanyika jana katika hoteli ya Serena
jijini Dar es Salaam. Mmoja
ya wazazi waliohudumiwa na taasisi ya Global Education Link wakitoa
ushuhuda wao jinsi watoto wao walivyowezeshwa kutafutiwa nafasi za
masomo kwa vyuo vya nje ya nchi bila usumbufu kwa vyuo vinavyotambuliwa
na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania. Ambapo wazazi hao walitoa rai yao kwa
wazazi wengine kuendelea kuiunga mkono GEL ili isonge mbele zaidi kwa
vile inafanya kazi zake kiuhakika bila ya kudanganya. Mkurugenzi
wa Elimu ya juu, Wizara ya Elimu na mafunzo ya Ufundi, Profesa Sylvia
Temu ambaye alikuwa mgeni rasmi aliyemwakilisha Waziri wa Elimu na
mafunzo ya Ufundi (katikati) akizindua. Pembeni toka kulia ni
Wafanyakazi wa GEL, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Afrika Tanzania,
Ammish OWUSU-AMOA, Kaimu Katibu mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania,
Profesa Magishi Nkwabi Mgasa pamoja na Naibu katibu mkuu Tamisemi,
Zuberi Samataba. Hiki ndicho kilichozinduliwa.
Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.