IMANI ya
kuabudu inayotiliwa shaka duniani ya Freemason imetajwa kuwa nyuma ya
pazia la ajali mbaya ya Basi la Sumry iliyotokea katika Kijiji cha
Ulyampiti mkoani Singida mwanzoni mwa wiki iliyopita na kusababisha vifo
vya watu 19, wakiwemo polisi wa usalama barabarani wanne.
Basi la Sumry lililopata ajali mbaya iliyotokea katika Kijiji cha Ulyampiti mkoani Singida mwanzoni mwa wiki iliyopita.
Habari za
uhakika kutoka kijijini hapo zinasema siku moja baada ya ajali hiyo
mbaya, basi moja linalosafiri kati ya miji ya Bukoba na Dar es Salaam
(jina linahifadhiwa) lilipita katika kijiji hicho na kutupa karatasi
zilizokuwa na maneno ya kuwahamasisha watu kujiunga na dini hiyo
inayodaiwa kuwa ya kishetani.
Inadaiwa
kuwa kwenye karatasi hizo kulikuwa na mchoro unaoaminika kutumiwa na
watu wa dini hiyo ambapo pia ilichorwa michoro yenye kuonesha burungutu
la fedha, sanjari na namba za simu zinazowataka watu kuzitumia endapo
watataka kujiunga.
Baadhi ya watu waliopoteza maisha kutokana na ajali hiyo.
Tulipoziona
zile karatasi na kuzisoma, wengi tulikimbia kwa sababu tunahusisha
kabisa na ajali ya Sumry. Mbaya zaidi ajali yenyewe inatia shaka. Mimi
nilipoambiwa kuhusu hizo karatasi, sikutaka kuziona, nikakimbia,î
alisema mwanamke mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Yasinta, mkazi wa
kijiji hicho.
Alisema karatasi hizo zilitupwa pia katika Vijiji vya Isuna, Nkuhi, Samumba na Ikungi wakati basi hilo ambalo mara kwa mara huripotiwa kupata ajali, likiwa katika safari yake kuelekea Dar es Salaam.
Kijana mmoja
aliyejitambulisha kwa jina la Zuberi ambaye hufanya shughuli zake
katika stendi ya mabasi Kijiji cha Ulyampiti alithibitisha kutupwa kwa
karatasi hizo na yeye alikuwa nayo mkononi.
ìNi kweli
hizo karatasi zimetupwa, hata washikaji wa vijiji vya jirani nao
wametuambia wameokota, mimi mwenyewe hapa nilipo ninayo, ina namba za
simu ambazo wanasema tuwasiliane nao kama tunataka kujiunga,î alisema
kijana huyo na kutaja namba hizo, ambazo hata hivyo haziwezi kuandikwa
gazetini kwa sababu maalum.
Wanakijiji
hao walikwenda mbali zaidi na kudai kuwa basi lilitupa karatasi hizo pia
limechorwa alama inayodaiwa kutumiwa na watu wa imani hiyo katika moja
ya sehemu za gari hilo ambalo hata hivyo, gazeti letu linaendelea
kufuatilia kwa karibu sakata hilo ili kujiridhisha.
Ajali ya
Basi la Sumry ilitokea Jumatatu iliyopita majira ya usiku, baada ya gari
hilo kuacha njia na kulifuata kundi la watu lililokuwa pembeni
likishuhudia askari polisi wakiuchukua mwili wa mtu mmoja aliyegongwa na
gari akiwa katika pikipiki.
Inadaiwa
kuwa kipande ambacho ajali hiyo imetokea kimekuwa na matukio mengi ya
kushangaza, kwani mara nyingi zinatokea ajali za kushangaza ambazo
katika kipindi cha miaka minne sasa, watu zaidi ya 50 wamepoteza maisha
katika maeneo ya jirani ya
vijiji hivyo.
-gpl
vijiji hivyo.
-gpl