Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
RAIS
wa shirikisho la soka nchini Tanzania, Jamal Malinzi imepigana kiume
kuwasiliana na mwenyekiti na mmiliki wa klabu ya TP Mazembe, Moise
Katumbi na taarifa njema juu ya mawasiliano hayo ni kwamba
washambuliaji wawili wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta na
Thomas Ulimwengu watawasili jumamosi mchana kwa ajili ya mchezo wa
jumapili.
Taarifa
za uhakika kutoka ndani ya TFF zinaeleza kuwa Rais Malinzi
amethibitisha ujio wa wanandinga hao tegemeo kwa Taifa stars na kuibua
matumaini ya Taifa stars kufanya vizuri kwasababu Samatta na Ulimwengu
ni wachezaji mahiri zaidi kwa sasa.
Nyota
hao wawili watatumiwa kwa mara ya kwanza na kocha wa Taifa stars, Mart
Nooij katika mechi ya raundi ya awali kuwania kufuzu fainali za mataifa
ya Afrika mwakani nchini Morocco dhidi ya Zimbabwe kwenye uwanja wa
Taifa, jijini Dar es salaam.
TP
Mazembe aliwazuia wachezaji hao kuja Tanzania kwasababu wanawahitaji
katika michezo ya makundi ya ligi ya mabingwa barani Afrika.
Matajiri
hao wa DRC walipo kundi A wanatarajia kucheza mechi ya
kwanza dhidi ya El Hilal Omduran siku ya ijumaa mjini Khartoum nchini
Sudan, hivyo baada ya mechi hiyo wachezaji hao wa Tanzania watatua
nchini jumamosi na kucheza mechi siku ya jumapili.
Hata
hivyo baada ya mechi hiyo watakwea pipa kuelekea Lubumbashi DRC tayari
kwa maandalizi ya mechi ya pili dhidi ya mahasimu wao AS Vita mei 25
mwaka huu.
Baada
ya mechi hiyo na AS Vita ambapo wiki iliyopita walikutana nao katika
mchezo wa mwisho wa ligi kuu ya DRC na kushuhudia vurugu kubwa
ziliosababisha watu zaidi ya 15 kupoteza maisha, Samatta na Ulimwengu
wataweza kupata nafasi ya kucheza mechi ya marudiano na Zimbabwe mjini
Harare.