STAA wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper amefunguka kuwa tangu aanze kujihusisha na masuala ya mapenzi hajawahi kulia.
Staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper
Akizungumza
na mwanahabari wetu, Wolper ambaye ana muonekano wa ‘kigumu’, alisema
siku zote anaamini katika kupambana hivyo hawezi kumlilia mwanaume hata
iweje.
“Sijawahi
kulia pale nilipoachwa wala kuachana na mwanaume, akili yangu yote
inaamini katika kutafuta maisha hivyo siwezi kujirahisisha nikamwaga
machozi kwa ishu za mapenzi,” alisema Wolper.