Mbuva, akiwa na majeraha usoni baada ya kumwagiwa mafuta ya moto.
MWANADADA aliyefahamika
kwa jina moja la Mbuva, mkazi wa Gongo la Mboto jijini Dar, hivi
karibuni amejikuta akiharibiwa uso wake kwa kumwagiwa mafuta ya moto na
shosti wake aitwaye Mama Sofia, kisa kikidaiwa ni mume wa mtu. Tukio
hilo lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo inadaiwa mama Sofia
alimfanyia mwenzake unyama huo akimtuhumu kutembea na bwana
wake.Akisimulia ilivyokuwa, Mbuva alisema: “Mama Sofia alipewa maneno ya
uongo kwamba akiwa safarini eti nilitembea na bwana wake.
“Siku ya tukio alinipigia simu akaniita
kwake, nilikuwa sipajui ila akanielekeza, ile nafika tu majirani zake
wakamwambia mimi ndiye nilikuwa nakwenda kulala pale na mume
wake.“Nikajaribu kujitetea lakini hakunielewa. Nikaondoka, baadaye
akaniita tena, kufika pale nikakuta ugomvi kati ya mama Sofia na mumewe,
ghafla mama Sofia akatoka akiwa na kikombe cha mafuta ya moto
akanimwagia usoni.
“Nikaanza kupiga kelele, watu
wakajaa ndipo tukachukuliwa wote na kupelekwa katika Kituo cha Polisi
cha Mazizini na tukaandikisha, mimi nikakimbizwa hospitali. Ameniharibu
uso wangu bila kosa, Mungu atanilipia kwani naamini malipo ni hapahapa
duniani.”
Mama Sofia hakuweza kupatikama mara moja kuzungumzia tukio hilo.