MWENYEKITI WA KITONGOJI ASAKWA KWA KUMILIKI SHAMBA LA BANGI

#HABARI MWENYEKITI WA KITONGOJI ASAKWA KWA KUMILIKI SHAMBA LA BANGI

Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro linamsaka Mwenyekiti wa serikali ya kitongoji kimoja katika kata ya Kahe, wilaya ya Moshi kwa tiketi ya CCM, ambaye ametokomea kusikojulikana baada ya wananchi kufichua shamba la bangi lenye ukubwa wa robo ekari analomiliki.

Mbali ya shamba hilo kugunduliwa, nyumbani kwa kiongozi huyo polisi pia walikamata kilo 30 za bangi, ambazo zilikuwa mbioni kusafirishwa  kwenda kuuzwa katika maeneo mbalimbali nchini. 

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz, jana alisema makachero wa jeshi hilo wanamtafuta kwa udi na uvumba mwenyekiti huyo, ambaye amekimbia baada ya kubaini anatafutwa kwa kosa la kulima bangi na kuhifadhi dawa hizo za kulevya nyumbani kwake kinyume cha sheria za nchi. 
“Bado tunamtafuta huyu mwenyekiti lakini pia katika msako ulioendelea siku hiyo pia tulimbaini mkulima mwingine ambaye ana shamba la bangi robo ekari katika kijiji cha Kisange Sangeni, kata ya Kahe. Hawa wote wawili wamepanda na kustawisha bangi katikati ya shamba la mahindi

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...