Staa wa muziki wa Kizazi Kipya, Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ au ‘Jide’ akiwa na mumewe Gardner G. Habash wakati wa harusi yao.
HABARI kubwa
ya mjini hivi sasa, hasa kwenye mitandao ya kijamii ni juu ya madai
mazito ya kuvunjika kwa ndoa ya selebriti wawili Bongo, staa wa muziki
wa Kizazi Kipya, Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ au ‘Jide’ na mtangazaji
maarufu wa Radio Times FM, Gardner G. Habash, iliyofungwa Mei 14, 2005,
Ijumaa linamaliza utata.
KABLA
Kabla
ya Gardner kufunguka, habari zilidai kwamba wawili hao walikuwa kwenye
gogoro zito ambapo Gardner aliamua kuondoka katika nyumba waliyokuwa
wakiishi pamoja iliyopo Kimara-Temboni, Dar.
Ilidaiwa kwamba baada ya kuondoka nyumbani eti Gardner alikwenda kukaa kwa mmoja wa ndugu zake.
Habari
hizo za kwenye mitandao ambazo hazitaji chanzo cha kuvunjika kwa ndoa
hiyo, zilidai watu wa karibu na familia hiyo walisema hiyo siyo mara ya
kwanza kwa wawili hao kutengana, lakini mzozo wa safari hii unaweza
ukawa wa moja kwa moja.